dc.contributor.author | Mutuku, Perlice N | |
dc.date.accessioned | 2021-08-20T07:57:19Z | |
dc.date.available | 2021-08-20T07:57:19Z | |
dc.date.issued | 2015 | |
dc.identifier.uri | http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155292 | |
dc.description.abstract | Lengo la utafiti huu limekuwa kuchanganua ubanifu wa fani katika hadithi fupi katika
diwani ya Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine (2011) iliyohaririwa na Iribemwangi.
Mada imechaguliwa kwa misingi kuwa kazi ya kifasihi huzua maana kamili
inapochunguzwa kimuundo na kifani. Aidha hadithi fupi zilizoteuliwa hazijawai
kufanyiwa uhakiki wa kifani kwa mtazamo wa nadharia ya elimu mitindo. Utafiti wetu
umelenga kuchunguza ubanifu katika usawiri wa wahusika na kubainisha nafasi ya
matumizi ya lugha katika diwani husika. Nadharia ya elimu- mitindo imetumika katika
uchanganuzi wa usawiri wa wahusika na uchambuzi wa kimtindo na imefaa utafiti huu
kwa kutoa picha inayodhihirisha baadhi ya sifa za hadithi fupi za kimtindo na kifani
kama zinavyodhihirika katika diwani ya Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine.
Madhumuni yanayorejelewa yametumiwa kuunda maswali ya utafiti ambayo
yametuongoza katika uchanganuzi wa usawiri wa wahusika na uchambuzi wa kimtindo
katika diwani hii. Matumizi ya lugha katika diwani husika yamegunduliwa kusheheni
methali, semi, tamathali za usemi, sentensi fupi, sentensi ndefu, dayolojia na monolojia.
Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa matumizi ya lugha yamechangia dhamani ya
kiujumi katika hadithi mahsusi na pia kuonyesha namna uhuru wa kutumia lugha katika
uandishi huacha athari fulani iliyonuiwa. Utafiti huu pia ulidhihirisha kuwa wahusika
katika diwani hii ni wahusika wa mraba mmoja. | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | university of Nairobi | en_US |
dc.rights | Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States | * |
dc.rights.uri | http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/ | * |
dc.subject | Ubanifu Wa Fani | en_US |
dc.title | Ubanifu Wa Fani Katika Diwani Ya Alidhani Kapata Na Hadithi Nyingine | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |