Nafasi ya Dini katika jamii ya kisasa kama ilivyosawiriwa katika Riwaya za Nguvu ya Sala, Walenisi na Babu alipofufuka
View/ Open
Date
2005Author
Karanja, Eddah, W
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika kazi hii tumezihakiki nwaya za Nguvu ya Sala (1995) ya K.W Wamitila,
Walenisi (1998) ya K. vlkangi na Babu Alipofufuka (2003) ya SA. Mohamed.
Tumeangalia jinsi waandishi hawa wamelishughulikia swaJa la dini na kuonyesha nafasi
yake katika jarnii ya kisasa.
Uhakiki huu umegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza tumeelezea somo la
utafiti, madhurnuni, sababu za kulichagua somo hili, rnipaka na upeo na yaliyoandikwa
kuhusu swala la dini. Aidha tumeeJezea misingi ya kinadharia iliyotumiwa katika utafiti
huu. Pia tumeelezea njia tulizozitumia katika utafiti wetu.
Katika sura ya pili, tumeangalia jinsi dim ilivyosawiriwa katika riwaya ya Nguvu ya Sala.
Tumeonyesha jinsi athari mbalimbali za dini zilivyojitokeza katika riwaya hasa katika
kizazi kipya. Tumeonyesha jinsi wakati mwingine utamaduni wa wanaj ami i unavyopata
ushindi ukilinganishwa na dini.
Katika sura ya tatu, turneshughulikia dini katika riwaya ya Walenisi. Hapa tumeonyesha
jinsi dim ilivyotumiwa na inavyotumiwa kuwalainisha na kuwadhulumu watu na
kuwajaza kasumba ya maisha merna ya baadaye huko Peponi huku wakiteseka duniani.
Katika sura ya nne, tumechunguza dim katika riwaya ya Babu Alipofufuka ambapo
tumeonyesha jinsi ukengeushi unavyoweza kuwafanya wakwasi waidharau dini kiasi
cha kujitoshanisha na miungu
Sura ya tano ni hitimisho na mapendekezo.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: