• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchambuzi linganishi wa maudhui na mtindo baina ya ngano za waswahili na wakuria

    Thumbnail
    Date
    1987
    Author
    Marwa, Miriam B
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii ni Uchambuzi linganishi wa Mtindo na maudhui baina ya ngano za Waswahili na Wakuria. Hivyo basi huu ni uchambuzi wa fasihi simulizi, ambapo tunashughulikia ngano peke yake. Fasihi simulizi inazo tanzu nyingi, baadhi yake ni nyimbo, vitendawili na ushairi.Tanzu hizi zaweza kujisimamia zenyewe. Kwa sababu hii hatuwezi kuzichambua zote kwa pamoja. Hata hivyo ni muhimu kujua kwamba, tanzu za fasihi siruulizi huingiliana. Kwa mfano katika ngano kuna nyimbo mara kwa mara. Mahusiko yetu katika ngano hizi, ni kuchambua maudhui na mtindo. Tusemapo mtindo, tunamaanisha usanifu wa lugha inayotumiwa na wasimulizi wa ngano ili waweze kuwasilisha ujumbe wao kwa wasikilizaji. Maudhui kwa upande mwingine ni ule-ujumbe unaotolewa kwa ajili ya jamii. Kwa kuwa fasihi simulizi kama fasihi andishi inamhusu binadamu, kigezo tutakachotumia kupimia kazi hii ni msingi wa nadharia ya ki-Marx. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unaeleza mahusiko yetu katika tasnifu hii. Pia inaonyesha sababu za kulichagua somo hili, yaliyoandikwa kuhusu mada ya kazi hii na njia za utafiti zilizoturniwa kufanya utafiti wenyewe. Sura ya pili ni ucharnbuzi wa ngano za Waswahili na Wakuria. Kabla ya uchambuzi, kuna utagulizi ambao unae1eza mahusiko yetu katika sura hii, pamoja na kueleza kwa muhtasari tu, uhusiano ulioko baina ya mtindo na maudhui. Baada ya utangulizi huo, tunaingilia uchambuzi wenyewe. Uchambuzi huu, umegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza imechukua uchambuzi wa ngano za Waswahili. Ngano hizi ni kama zifuatavyoi (1) Sungura na Fisi (2) Kinungu Maria (3) Mtu na Mkewe Sehemu ya pili imechukua uchambuzi wa ngano za Wakuria. Ngano hizi ni kama zifuatavyoi: (1) Mama na Sungura (2) Wesanganache (3) Nyanya na watoto Sura ya tatu ni ulinganismwa maudhui na mtindo wa ngano ambazo tumezichambua. Kabla ya ulinganishi wenyewe. Kuna utangu1izi ambao unaeleza sababu za kuwa na ulinganishihuu. Ulinganismhuu umegawanyika katika sehemi mbili. Sehemu ya kwanza imechukua kufanana kwa maudhui na mtindo baina ya ngano za Waswahili na Wakuria. Sehemu ya pili imechukuwa tofauti zilizoko baina ya ngano za jamii hizi, tukizingatia maudhui na mtindo. Baada ya ulinganishi huu, tuna hitimisho. Katika hitimisho uamzi na mapendekezo yetu yanajitokeza Mwisho kabisa kuna ambatisho ambalo ni uambatanishi wangano zote tulizozichambua. Ngano hizi zimepangwa kama ifuatavyo kwanza kuna ngano za Waswahili, zikifuatiwa na ngano za Wakuria katika lugha ya Kikuria. Mwisho ni tafsiri ya ngano za Wakuria katika lugha ya Kiswahili.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/16066
    Sponsorhip
    University of Nairobi
    Subject
    Ngano za waswahili
    Uchambuzi linganishi
    Wakuria
    Maudhui na mtindo
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback