Show simple item record

dc.contributor.authorJoseph, Ruth N
dc.date.accessioned2023-02-18T07:43:27Z
dc.date.available2023-02-18T07:43:27Z
dc.date.issued2022
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/162612
dc.description.abstractKatika utafiti huu wetu tumeshughulikia taswira ya jagina kwa kuwarejelea majagina Nabii Isa kama alivyoelezwa katika Utenzi wa Nabii Isa, wake Musa Mzenga (1977), na Sundiata katika Utenzi wa Sundiata ulioandikwa na Djibril Tamsir Niane (1960). Lengo letu kuu katika utafiti huu lilikuwa kulinganisha sifa za kijagina za Nabii Isa na Sundiata kwa nia ya kudhibitisha kuwa sifa za majagina waliosawiriwa katika aina mbili za kazi za kifasihi na waliotoka maeneo tofauti ya kimazingira zinaweza kufanana. Katika sura ya kwanza ni tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, maswali ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, msingi wa kinadharia, yalioandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia historia ya Nabii Isa na Sundiata pamoja na historia ya jamii zilizowazaa na kuwakuza. Katika sura ya tatu tumezinganisha sifa za kijagina za Nabii Isa na Sundiata. Sura ya nne tumeshughulikia umuhimu wa Nabii Isa na Sundiata katika jamii zao. Sura ya tano ni hitimisho ambapo tumeangazia matokeo ya utafiti na mapendekezo kuhusu utafiti wa baadaye. Utafiti wetu umeongozwa na nadharia ya vikale tukijikita hasa katika mtazamo wake Northrop Frye.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleTaswira Ya Jagina: Ulinganishi Wa Nabii Isa Na Sundiataen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States