Lugha Mkakati Na Utambulisho Wa Kijamii Wa Familia Za Mitaani Jijini Nairobi: Kifani Cha Mtaa Wa Mathare
Abstract
Utafiti huu unaangazia matumizi ya lugha katika mawasiliano ya wanafamilia wa mitaani mtaani Mathare, Nairobi. Utafiti huu ulinuia kujenga uelewa wa jinsi muktadha unavyoathiri utambulisho na mazungumzo yao. Kupitia uchambuzi wa muktadha wa lugha, tulibaini kuwa wanafamilia hawa hutumia lugha kimkakati na pia hubadilisha lugha kutegemea malengo yao ya wakati husika na muktadha wa mazungumzo. Utafiti huu ulizingatia malengo matatu: kufahamu jinsi muktadha unavyowatambulisha na kutimiza malengo yao, kutathmini athari ya muktadha wa mazungumzo kwenye utambulisho wao, na kufafanua matumizi ya lugha katika mada ambazo hutawala mazungumzo yao. Wanafamilia wa mitaani walionyesha uchanganyaji wa lugha na uwezo wa kutumia lugha mbalimbali kulingana na hali ya mazungumzo. Mada zilizotawala mazungumzo yao ni makuzi na dhuluma, na lugha iliyochaguliwa ilitegemea muktadha. Utafiti huu ulitegemea uchunguzi shiriki na uchanganuzi wa mazungumzo yao, huku sampuli ikianza na familia moja ya kupanga na kupanuka kadri utafiti ulivyoendelea. Kazi hii imepangiliwa katika sura tano ambapo tulijikita kwa malengo ya utafiti wetu huku tukiongozwa na mihimili ya nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles na ile ya Leech kuhusu uchanganuzi mitindo. Tulijikita kwa muktadha sahili, muktadha changamano na muktadha unaohusiana na janga. Tuligundua kuwa makutano ya kilugha baina ya watafitiwa hujitokeza zaidi watafitiwa wanapotaka kuficha siri zao dhidi ya wanakundi-nje. Vilevile, mwachano wa kilugha hauwezi kuepukika wakati watafitiwa wametofautiana. Tulichanganua data yetu na kisha kuiwasilisha kimaandishi kwa matumizi ya lugha nathari yenye mijadala na ufafanuzi kwa kuzingatia madhumuni na malengo ya utafiti huu.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [979]
The following license files are associated with this item: