• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Sanaa Katika Tafsiri: Matatizo Na Athari Zake

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (2.144Mb)
    Date
    1997
    Author
    Mutie, Edith K
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Kazi nyingi za tafsiri hudharniria kuiboresha tafsiri na athari zake katika Kiswahili; ikizingatia matatizo, makosa, dosari na athari zake juu ya fasihi kwa jumla. Uhakiki huu umejikita katika kazi moja ya kifasihi ambayo irnetafsiriwa katika Kiswahili, Mizigo, (1977) iliyofanywa na Bi. A. Muro. Tuliangalia kazi hii tafsiri huku tukiilinganisha na kazi asilia, The Burdens ya John Ruganda kwa kuchunguza athari za mtindo katika tafsiri. Tulifanya hivi kwa sababu tuliamini ya kuwa dosari zilizoko katika kazi hii zinajitokeza pia katika kazi zote za fasihi tafsiri. Ni jambo lisilowezekana kuziangalia kazi zote za tafsiri zilizoko katika Kiswahili. Kazi hii tunatumaini ya kuwa itakuwa kielelezo cha yanayohusika katika kitendo cha kutafsiri kazi nyengine za aina hii. . >(tl1lA / I O\T~iri hii irnegawika katika sura nne, kila moja ikijadili kipengele maalumu juu ya kitendo cha kutafsiri kwa mujibu wa fasihi. Kila sura ina hitirnisho ambapo maoni na msirnamo wa tasnifu hii umetolewa kwa mujibu wa yanayojitokeza katika utafiti. Sura ya kwanza ni utangulizi unaobainisha kiini cha utafiti kuhusu sanaa katika tafsiri. Katika sura hii tumeangaza umuhimu wa kufanya uchunguzi kuhusu kitendo cha kutafsiri. Kuna pia madhumuni, misingi ya nadharia, upeo wa tasnifu, sababu za kuchagua somo na jinsi utafiti utakavyofanywa. Sura ya pili inajadili matatizo ya tafsiri kwa jumla na jinsi yanavyochangia katika kupotoka kwa sanaa katika tafsiri. Inaangalia dhana ya tafsiri na kufafanua pamoja na kujadili athari za kila mojawapo ya matatizo hayo kwa sanaa ya makala pokezi. Haya yote yamefanywa kwa ajili ya kuweka misingi thabiti na bora ya uhakiki wa kazi iliyoteuliwa. Sura ya tatu ni uhakiki halisi wa makosa ya kisanaa katika kazi ya Mizigo. Katika sura hii, uhakiki umefanywa kwa mujibu wa misingi ya kinadharia iliyojadiliwa katika sura iliyotangulia. Dosari mbalimbali za kisanaa zinazijitokeza zimetajwa, hali kadhalika matatizo yaliyomkabili mtafsiri. Mambo hayo yote yamechukuliwa rnifano tu ya kuangazia uhalisi wa fasihi tafsiri kwajumla. Sura ya nne ni hitimisho inayotoa muhtasari wa maoni kutokana na utafiti. Maoni ya jumla, mapendekezo ya utafiti mpya na msimamo wa tasnifu umebainishwa.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18189
    Citation
    T asnifu hii imetolew a ill kutosheleza baadhi y a mahit all y a shahada y a m.a. ka tika chuo kikuu cha Nairobi
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Department of Arts
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback