• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Fani katika ushairi wa Hassan Mwalimu Mbega: uhakiki wa upisho wa umalenga na dafina ya umalenga

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (5.653Mb)
    Date
    1997
    Author
    Osiemo, Donald O
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii imeshughulikia fani katika ushairi wa Hassan Mwalimu Mbega. Tumehakiki diwani zake mbili ambazo ni Upisho wa umalenga (1975) na Dafina ya Umalenga (1984) kwa kutumia nadharia ya urasimu. Kuna sura tano katika tasnifu. Sura ya kwanza ni ya utangulizi ama pendekezo la utafiti. Ni sura inayohusu somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, sababu za kulichagua somo, haipothesia, yaliyoandikwa kuhusu somo, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Sura ya pili ambayo ni ya misingi ya uhakiki inahusu uamili wa lugha ya kishairi katika sanaa, sifa zake, na namna inavyoshirikiana au kutumiwa katika ploti. Tumeangalia umuhimu wa kila mojawapo ya vipengele hivyo na mchango wao katika fani kwa jumla. Baada ya kuangalia mengi ya kifani ambayo ni mwongozo wa sura zinazofuatia, tumezitamzama na kuzihakiki tungo za mwalimu Mbega katika misingi ya yaliyopitiwa katika sura za kwanza na pili. Maswala ya nadharia ya urasimu na mwongozo wake vimezingatiwa katika kuhakiki tungo hizo. Sura ya tatu inahusu uhakiki kifani wa upisho wa umalenga, huku sura ya nne ikishughulikia maswala ya kifani katika diwani ya Dafina ya Umalenga. Sura ya tano ni hitimisho ambapo kwa njia ya muhtasari imethibitisha haipothesia pamoja na kushughulikia maswala mengine ya kifani. Tasnifu hii ina sura tano zinazoshughulikia maswala ya kifani. Kwa sababu ambazo hatukuweza kuziepuka, alama za kufungia maneno zimetokea zikiangalia upande mmoja. Hii ni kwa sababu, ya aina ya kompiuta iliyotumiwa ambayo haina alama za kufungia. Tunaomba radhi kwa makosa hayo .
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18351
    Citation
    Masters of education thesis,University of Nairobi (1997)
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Department of Arts
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback