• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uhakiki wa fani katika tamthilia za K.W. Wamitila

    Thumbnail
    View/Open
    Abstract (11.08Kb)
    Date
    2005
    Author
    Kahiro, Duncan M
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii ni uhakiki wa fani katika tamthilia za Kiswahili ambazo zimetungwa na Wamitila, K.W. Tamthilia hizi ni Wingu La Kupita (1999) na Pango (2003). Katika tahakiki yetu, tumeteua na kujadili vipengele maalum vya fani. Kazi ina sura tano. Katika sura ya kwanza, tumeelezea dhana za kimsingi zinazohusiana au kupatikana katika somo hili. Dhana hizi ni pamoja na: fani na tamthilia. Tumeelezea pia msingi wa kinadharia tulioutumia, sababu za , kuchagua mada hii na upeo na mipaka yake. Tumeweza kurejelea kazi za fasihi zilizowahi kuandikwa zikiangazia fani. Sura ya pili ni kuhusu ujumla na mjengo wa ploti. Katika sura hii tunaeleza dhana ya ploti. Vipengele ambavyo tumejadili ni mfululizo wa vitushi na jinsi vinashirikiana katika kuleta umoja wa kazi na tumetoa tathmini yetu kuhusu ploti katika kila tamthilia. Katika sura ya tatu tumeshughulikia umbuji wa wahusika. Tumejadili jinsi wahusika mbalimbali walivyochorwa katika tamthilia, nafasi au majukumu yao na mchango wanaotoa katika uendelezaji wa kazi. Katika sura ya nne, tumehakiki matumizi ya lugha katika kazi za Wamitila. Tumeangalia jinsi lugha imetumiwa katika mazingira mbalimbali na inavyotumiwa na wahusika wa urnri mbalimbali.Tumejadili pia usanaa na ujumi wa lugha iliyotumiwa. Sura ya tano ni ya hitimisho na mapendekezo. Katika sehemu hii tumeangaza kimukhtasari zile sifa baininifu zinazojidhihirisha katika ujumla wa fani katika kazi za Wamitila kama tulivyoweza kuzijadili na kuzihukumu. Uhakiki wetu umechambua udhaifu au ufanifu wa mtunzi katika umbuji wa wahusika na lugha. Tumeweza kutoa mapendekezo katika tasnifu kuhusu kazi tuliyoifanya.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18367
    Citation
    Master of Arts
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Faculty of Arts Kiswahili
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback