• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Ugatuzi wa utamaduni wa kikoloni katika tamthilia za Ngugi Wa Thiong'o

    Thumbnail
    Date
    2006-06
    Author
    Ng'ang'a , Samuel Irungu
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tahakiki nyingi za kazi za kifasihi za Kiswahili ambazo zimefanywa kuhusiana na ukoloni na ukoloni rnambo-leo zimejikita katika nadharia ya U-Marx. Tahakiki za aina hiyo hubakia kuangazia suala la uhusiano wa kiuchumi kama kitovu cha harakati za ukoloni na ukoloni mambo-leo. Kwa namna hiyo mahusiano ya kitamaduni katika miktadha hiyo hufumbiwa macho. Utafiti huu ulitiwa chachu na ukweli huo pamoja na kwamba ukoloni wa kitamaduni ulitangulia ule wa kiuchumi. Ni kupitia kwanza kuwatawala watu kitamaduni ambapo kuwaondoa kutoka kwa mfumo wao wa kiuchumi (waliouzoea) hadi katika mfumo mpya wa kiuchumi (wa watawala) huwezekana. Utafiti huu umezishughulikia tamthilia za Ngugi wa Thiong'o kwa kuzingatia ukweli huo. Katika sura ya kwanza, masuala ya kimsingi kuhusiana na utafiti yameshughulikiwa. Haya ni utangulizi, tatizo la utafiti, nadharia tete, madhumuni, msingi wa kinadharia, upeo na mipaka, fasili za istilahi zilizotumiwa kwa muktadha wa utafiti huu na yaliyoandikwa kuhusiana na somo hili. Sura ya pili imeshughulikia masuala ya lugha, fasihi, utamaduni, ukoloni na ubaadaukoloni. Upembuzi wa kina umefanywa katika kubainisha uhusiano uliopo kati ya dhana hizo. Sura hii imeyaangazia masuala ya kimsingi kuhusiana na nadharia ya baada-ukoloni vilevile. Sura ya tatu na ya nne nazo zimeshughulikia uhakiki wa kazi husika. Sura ya tatu imeshughulikia tamthilia za Mtawa Mweusi na Kesho Wakati Kama Huu huku sura ya nne ikishughulikia tamthilia za Nitaolewa Nikipenda na Mzalendo Kimathi. Mwishowe katika hitirnisho, mapengo, mapendekezo na masuala muhimu ya ubaadaukoloni kuhusiana na tamthilia zinazoshughulikiwa yanayoibuka katika uhakiki yameangaziwa.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18405
    Citation
    Masters thesis University of Nairobi 1993
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Department of linguistics and African languages, university of Nairobi
     
    Description
    The information material is in Swahili language
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback