• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Kubadilisha msimbo katika bunge la Kenya

    Thumbnail
    Date
    2004-12
    Author
    Nandama, Sussy K
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Katika nchi ya Kenya, wazungumzaj i hutumia lugha ya Kiingereza ambayo ni lugha rasmi, lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya kitaifa na lugha za kienyeji. Kwa hivyo tunaona kuwa katika nchi hii mazingira ni ya uwingi lugha. Katika mazingira kama haya ubadilishaji msimbo hutokea. Vile vile ubadilishaji msimbo ni jambo ambalo hujitokeza bungeni kwa vile mazingira ya uwili lugha. Aghalabu wabunge wengi hubadilisha msimbo kutoka lugha ya Kiingereza hadi Kiswahili au lugha ya Kiswahili hadi Kiingereza. Hata hivyo wakati mwingine wao hubadilisha msimbo hadi lugha za kienyeji. Katika tasnifu hii tumezingatia ubadilishaji msimbo kutoka lugha ya Kiswahili hadi lugha ya Kiingereza. Tumechunguza sababu zinazowafanya wabunge kubadilisha msimbo, ni aina ipi ya kubadilisha msimbo hujitokeza wabunge wanapobadilisha msimbo na ni kwa kiwango kipi ambacho wao hubadilisha msimbo. Baadhi ya sababu zinazowafanya wabunge kubadilisha msimbo ni kama vile kutaka kutumia muda au maneno machache kueleza j ambo fulani, kunukuu, wabunge kuwa na mielekeo hasi kuhusu baadhi ya istilahi za Kiswahili na pia wao hubadilisha msimbo wanapotaja majina ya mashirika na vyama vya kisiasa. Katika utafiti huu -pia tumechunguza ama mbili za kubadilisha msimbo ambazo hujitokeza bungeni. Aina ya kwanza ni ubadilishaji msimbo -unaotokea baina ya sentensi na aina ya pili ni ubadilishaji msimbo ambapo wabunge hutumia lugha zaidi ya moja katika sentensi. Aina hii ya pili hujitokeza zaidi katika majadiliano ya bunge. Vile vile tumechunguza m kiwango kipi ambacho wabunge hubadilisha msimbo. Je, ni kwa kiwango chajuu, kadiri au kiwango cha chini.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18436
    Citation
    Nandama,K.S.(2004).Kubadilisha msimbo katika bunge la Kenya
    Sponsorhip
    University of Nairobi
    Subject
    Msimbo
    Bunge
    Kenya
    Description
    MA-Thesis
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback