• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Ufaaji wa Kiswahili kama lugha ya kisomo

    Thumbnail
    Date
    1991
    Author
    Likhako, Pamela Imbuhila
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Katika tasnifu hii, tumechunguza ufaaji wa Kiswahili kama lugha ya kufunzia katika viwango vyote vya elimu. Tumechunguza utoshelezaji wa Kiswahili katika kufunza hasa masomo ya Kisayansi na taaluma za kiufundi. Tumezingatia hasa Istilahi zilizoko katika masomo ya sayansi na ya kiufundi katika viwango vyote vya elimu na utoshelezaji wa hizi istilahi. Tasnifu hii imeonyesha kwamba Kiswahili kinatosheleza na kinafaa kama lugha ya kisomo. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni dibaji inayotanguliza kazi hii. Katika sura hii tumeeleza mada ya somo letu la utafiti na madhumuni ya tasnifu hiyo. Ni katika sura hii ambapo tunazijadili sababu za kuchagua somo hili, mipaka ya tasnifu hii na msingi wa nadharia tuliyotegemea katika utafiti wetu. Aidha tumejadili kazi za watu mbali mbali waliochunguza kazi inayohusiana na yetu na tukadokeza. na haipothesia zetu. Tumeihitimisha kazi hii kwa kuzieleza njia tulizozitumia katika utafiti huu. Katika sura ya pili, tumejadili hali ya lugha nchini Kenya. Tumejaribu kujadili sababu zinazofanya hali ya lugha kuwa ilivyo. Tumeangalia mfumo wa elimu ya 8.4.4 na athari zake hasa kwa lugha ya Kiswahili. Ni katika sura hii ambapo tumejadili lugha ya sayansi na pia kuchunguza sababu za kudhania kwamba Kiswahili chafaa kama lugha ya kisomo. Katika sura ya tatu tumegusia mashirika na watu mbalimbali wanaoshughulikia uundaji wa istilahi. Pia tumezungumzia njia zinazotumika kuundia istilahi na tukachunguza ubora na udhaifu wa kila njia. Katika sura ya Nne tulijishughulisha na kuchunguza istilahi zilizopo katika masomo tuliyoyachagua ya Kisayansi na ufundi katika viwango mbalimbali vya elimu yaani katika elimu ya msingi, elimu ya upili na elimu ya vyuo. Su~a ya tano ni hitimisho pamoja na kuchunguza matatizo yanayokikumba Kiswahili nchini Kenya.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/19234
    Citation
    M.A (Swahili) 1991 Thesis
    Sponsorhip
    University of Nairobi
    Publisher
    Depatment of Linguistics, University of Nairobi
    Description
    Master of Arts Thesis
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback