• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uhakiki wa usimulizi katika riwaya ya Walenisi ya Katama Mkangi

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (1.912Mb)
    Date
    2005
    Author
    Ong'ondi, Bogonko E
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii imeshughulikia uhakiki na unakidi wa riwaya ya Walenisi iliyoandikwa na marehemuMkangi na kutolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa tisaini na tano (1995). Kazihii tumeigawa katika sura sita. Katika sura ya kwanza, tumeweka wazi pendekezo la utafitikwa kuonyesha tatizo la utafiti, sababu za utafiti wenyewe, nadharia tete, msingi wakinadharia na mbinu za utafiti. Vilevile tumeshughulikia upeo na mipaka ya utafiti huu miongoni mwa vipengee vingine vya pendekezo. Sura ya piliinahusu mtazamo kama kipengee mojawapo cha usimulizi. Katikasura hii tumejadili na kuweka wazi maana ya mtazamo na kuonyesha tofauti baina ya mtazamo na usimulizi. Kadhalika, tumeshughulikia sawia mbalimbali za usimulizi katika riwaya ya Walenisi. Vilevile tumeonyesha aina za usimulizi najinsi zinavyodhihirika katika riwaya hii. Katika sura ya tatu, tumeshughulikia unenaji na fikira kama kipengee cha usimulizi. Tumejadili aina tofauti tofauti za unenaji na fikira na kutoa mifano ya kudhihirika kwao katika riwaya hii. Nayo sura ya nne, inaangazia wakati kama kipengeekimojawapo cha usimulizi. Katika sura hii, tumejadili maana ya wakati na umuhimu wake katika usmulizi. Pia tumeonyesha jinsi mbalimbali wakati hudhihirika katika hadithi. Katika sura ya tano, tumejadili mpangilio na uwasilishaji kama.kipengee cha usimulizi. Tumeonyesha wazi kuwa hadithi inaweza kuwa na mpangilio wa moja kwa moja au iwe na mpangilio changamano ambapo kuna uegemezaji. Katika riwaya hii kuna mtindo changamano amhapo tumeonyesha na kufafanua ni kwa nini Mkangi akatumia mtindo huu. Vile vile, katika sura hii, tumeonyesha jinsi hadithi ya Walenisi imewasilishwa ambapo kuna mimesia na daigesia kama mbinu za uwasilishaji hadithi. Tumehitisha katika sura ya sita kwa kurejelea tuliyoyajadili katika sura zote za awali kwa muhtasari tu. Kadhalika tumeelezea matokeo ya utafiti wetu pamoja na matatizo tuliyokumbana nayo tukifanya utafiti huu. Hatimaye tumetoa mapendekezo kuhusu mtalaa huu.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/19323
    Citation
    M.A (Swahili) 2005 Thesis
    Sponsorhip
    University of Nairobi
    Publisher
    Depatment of Linguistics, University of Nairobi
    Description
    Master of Arts Thesis
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback