• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Matatizo ya Leksikografia tafsiri: Tathmini ya Kamusi ya F. Johnson (1939)

    Thumbnail
    View/Open
    Abstract (1.305Mb)
    Date
    1996
    Author
    Mwangi, Patrick I
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu yetu imejengwakatika msingi unaoafiki kuwa kamusi za lugha mbilini kazi halisi za tafsiri. Tahakiki nyingiambazo tayari zimeandikwa kuhusu matatizo ya tafsiri zimeegemeazaidikatika fasihi na kazi za kidini. Sisi tunaonyesha kuwa hata kamusi za lugha mbili zina matatizo mengiya tafsiri katika ngazi mbalimbali za lugha. Tasnifu yenyeweimegawanywakatika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumelifafanua somo letu la utaflti ambalo ni leksikografia-tafsiri. Pia, tumeonyesha madhumuni yetu katika utafiti huu na sababu zilizotufanya tuchague somo hili. Fauka ya haya, tumeelezea upeo na mipaka ya tasnifu yetu na pia yaleyaliyoandikwa kuhusu somohili. Tumefafanua pia mwongozowa utafiti wetu na nadharia tete. Mwisho,tumeeleza njia tutakazozitumia katika utafiti wetu. Katika sura ya pili,tumeifafanua dhana ya tafsiri huku tukionyesha matatizo, umuhimu na nafasi yake. Aidha, tumeifafanua dhana ya leksikografia ambapo tumeeleza maana ya kamusi, mambo muhimu katika kamusi na aina za kamusi. Hatimaye tumeifafanua dhana ya leksikografia- tafsiri huku tukionyesha wale ambao hunufaisha na kamusi zalugha mbili. Mwisho,tumeonyesha nafasi ya maana katika tafsiri ya moja kwa moja, tafsiri-huru na tafsirimawasiliano. Sura ya tatu inahusu mambo ya sarufl katika kamusi za uwililugha. Tumeonyesha aina za sarufi, kisha tumefafanua kuhusu matatizo ya kifonolojiakatika kamusi zauwililugha na pia yaleya kimofolojiana kisintaksi. Hatimaye, tumetoa mifanoya tafsiri zisizosahihi kimofolojia na kisintaksi katika kamusi ya Johnson (1939)ya KingerezaKiswahiliambayo tunaitathmini. Sura ya nne ndiyo kiini c}?-akaziyetu. Tumeijadili ,dhana ya semantiki, maana katika semantiki na pia matatizo ya kisemantiki katika kamusi za uwililugha. Matatizo haya yanahusu uchaguzi wavisawe, uchanganuzi wa maana, maneno yajarnii rnojana ufafanuzi wa kimichoro na kimifano. Hatimaye tumeyaonyesha matatizo hayo kama yalivyojitokezakatika kamusi ya F.Johnson (1939). Tumeonyesha pia makosa ya kisemantiki katika mifano iliyotolewana mtunzi na matatizo mengineyajumla katika kamusi hiyo. Sura ya tano ni hitimisho. Tumeonyesha kwakifupiyaletuliyoyashughulikia, yaliyojitokeza kuhusu nadharia-tete, ufaaji wa mwongozo wetu wa utafiti, matatizo tuliyoyapata na kisha tunatoa mapendekezo yetu.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/19341
    Citation
    M.A (Swahili) 1996 Thesis
    Sponsorhip
    University of Nairobi
    Publisher
    Depatment of Linguistics, University of Nairobi
    Description
    Master of Arts Thesis
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback