• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Usawiri Wa Ndoa Katika Riwaya Ya Unaitwa Nani?

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (295.3Kb)
    Date
    2013-11
    Author
    Karinge, Joyce W
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Katika tasnifu hii, tumechunguza usawiri wa asasi ya ndoa katika riwaya ya Unaitwa Nani? ya K. W. Wamitila (2008). Tunatumia nadharia ya sosholojia ya fasihi kuihakiki riwaya hii. Tasnifu yetu ina na sura tano. Katika sura ya kwanza tumeeleza tatizo letu la uchunguzi, madhumuni ya utafiti wetu pamoja na nadharia tete. Tumeeleza sababu za kuchagua somo hili na misingi ya nadharia ya sosholojia. Hatimaye, tunachunguza yaliyoandikwa kuhusu somo hili, nadharia ya sosholojia ya fasihi na muhtasari wa riwaya ya Unaitwa Nani? (2008). Tumeeleza njia ambazo tumetumia katika utafiti wetu na mwishowe, hitimisho. Katika sura ya pili tumefiti jinsi asasi ya ndoa imesawiriwa katika riwaya ya Unaitwa Nani? (2008) kwa kuchanganua ndoa zilizoko katika riwaya husika na kutathmini mchango wa kila mwanandoa mhusika katika kuiimarisha au kuizorotesha ndoa yake. Katika sura ya tatu tumezichanganua changamoto zinazoikabili asasi ya ndoa kama zilivyosawiriwa katika riwaya ya Unaitwa Nani?. Katika sura ya nne tumechunguza mikakati ambayo jamii ya riwaya ya Unaitwa Nani? inatumia kuikomboa asasi ya ndoa isisambaratike. Sura ya tano imekuwa hitimisho la utafiti wetu. Tumetathmini kufaulu au kutofaulu kwa utafiti wetu kwa kutathmini matokeo ya uchunguzi wetu, ama yanalingana au hayalingani na madhumuni ya utafiti. Tumeangalia iwapo nadharia tete zetu zimethibitishwa kuwa za kweli au la. Tumetoa mapendekezo ya utafiti wa baadaye.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/58866
    Citation
    Karinge,Joyce W.;Novemba,2013.Usawiri Wa Ndoa Katika Riwaya Ya Unaitwa Nani?.
    Publisher
    University of Nairobi
     
    College of Humanities and Social Sciences
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback