• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Athari Za Kimofofonolojia Za Kiolusuba Katika Matumizi Ya Kiswahili Sanifu Kama Lugha Ya Pili

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (1.436Mb)
    Date
    2013
    Author
    Otiende, Merolyne A
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti huu una lengo la kuchanganua athari za kimofofonolojia za Kiolusuba katika matumizi ya Kiswahili Sanifu kama lugha ya pili. Utafiti huu umetumia nadharia ya FZA kuchambulia miundo ya lugha hizi mbili ili kuweka bayana athari hizo. Sura ya kwanza ni muhtasari wa jinsi utafiti huu ulikavyofanywa. Imeshughulikia utangulizi, madhumuni, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada hii, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia ulinganishi wa mifumo kamili ya fonimu za Kiswahili na Kiolusuba huku ikionyesha sifa bainifu za fonimu hizo. Aidha tumetoa mifano ya maneno yanayoundwa na fonimu hizo. Katika sura ya tatu, tumelinganisha na kulinganua miundo ya silabi katika Kiswahili na Kiolusuba. Katika sura ya nne, tumeshughulikia mambo mawili. Kwanza, tumeziorodhesha ngeli za nomino za Kiolusuba. Kisha, tumeshughulikia mifanyiko ya kifonolojia inayohusu irabu na konsonanti za lugha hizi mbili huku tukionyesha peo za mifanyiko hiyo. Data ya maneno yanayoonyesha baadhi ya athari za kisauti za Kiolusuba katika Kiswahili Sanifu imechanganuliwa katika sura ya tano. Maumbo sahihi yameonyeshwa huku maelezo yakitolewa kuhusu athari zenyewe. Katika sura ya sita tumetoa hitimisho pamoja na matokeo ya utafiti huu kwa muhtasari. Mwisho, tumetoa maoni na mapedekezo kuhusiana utafiti huu.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59341
    Citation
    Tasnifu hii imewasilishwa kwa ajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Nairobi. (2013)
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Faculty of Arts
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback