• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya mpya: babu alipofufuka (said Ahmed Mohamed) na watu wa Gehenna (Tom Olali )

    Thumbnail
    View/Open
    ABSTRACT.pdf (5.874Kb)
    Full Text (420.9Kb)
    Date
    2013-11
    Author
    Mwangi, Jedidah Wanjiru.
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii inahusu uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya za Said Ahmed Mohammed (Babu Alipofufuka) na Tom Olali (Watu wa Gehenna). Katika utafiti huu tumechunguza uhalisiajabu katika kiwango cha wahusika na mandhari katika riwaya hizi teule tukiongozwa na nadharia ya uhalisiajabu. Ili kufikia malengo yetu, utafiti huu umegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumetanguliza mada yetu, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, msingi wa nadharia, yalioyoandikwa kuhusu mada yetu, na njia za utafiti. Katika sura ya pili, tumechunguza hatua za mwanzo za uhalisiajabu ambazo ni uhalisia hakiki, uhalisia wa kijamaa hadi kufikia uhalisiajabu. Tumetambua ya kwamba waandishi waliotumia uhalisia kama vile Said A. Mohammed na K.W. Wamitila wamegeukia mtindo wa uhalisiajabu ili waweze kuyazungumzia mambo ambayo hawangeweza kuweka wazi kwa mtindo wa uhalisia. Katika sura ya tatu, tumechunguza na kubainisha vipengele vya uhalisiajabu katika viwango vya wahusika na mandhari yenye matukio ya uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Katika sura ya nne, tumebainisha wahusika na mandhari yenye matukio ya uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya ya Watu wa Gehenna. Katika sura ya tano, tumetathmini matokeo ya uchunguzi wetu kwa kurejelea madhumuni na nadharia tete zetu. Tumetoa hitimisho na mapendekezo ya utafiti wa baadaye.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59715
    Citation
    Tasnifu Hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Idara Ya Isimu Na Lugha, Chuo Kikuu Cha Nairobi
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Department of Linguistics and Languages
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback