• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Nafasi na utambulisho wa mwanamke katika natala na kifo kisimani

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (346.0Kb)
    Date
    2013-10
    Author
    Kipyegon, Keter E
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Madhumuni katika utafiti wetu yalikuwa ni; kwanza kuchunguza taswira chanya ambazo mwandishi anaangazia kumhusu mwanamke katika Natala na Kifo Kisimani. Pia, tulichunguza changamoto zinazokabili mwanamke katika harakati zake za kujikomboa. Katika kufikia madhumuni yenyewe, tulihitajika kusoma kwa mapana, kuhakiki na kuvichambua vitabu vinavyohusu nafasi ya mwanamke. Pia, tulihitajika kusoma vitabu vinavyoangazia nadharia ya Ufeministi. Katika utafiti wenyewe, tuliongozwa na nadharia ya Ufeminsiti wa Kiafrika. Kwa ujumla, nadharia ya Ufeministi ni nadharia yenye malengo maalum. Hulenga kuangalia na kujaribu kutatua matatizo yanayowakabili wanawake katika jamii ya ki-ubabe-dume. Kutokana na utafiti wetu, ilibainika kuwa Kithaka wa Mberia amefaulu vilivyo kumsawiri mwanamke katika jamii ya ki-ubabedume. Anaonyesha nafasi chukivu anayopewa mwanamke katika jamii ya aina hii. Licha ya hayo, mwandishi anatoa mchango wake muhimu katika kumjenga mwanamke kihadhi. Tasnifu yenyewe ina sura tano: sura ya kwanza inaangazia somo la utafiti, sura yenyewe lina utangulizi, tatizo la utafiti, madhumuni, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mpaka ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na njia za utafiti. Sura ya pili inaangazia nafasi na utambulisho wa mwanamke kama unavyodhihirika katika Natala (1997). Sura yenyewe inadokeza nafasi dhalilishi na dunishi katika sehemu ya kwanza, na nafasi chanya katika sehemu ya pili. Sehemu ya tatu ni hitimisho. Sura ya tatu inahusu nafasi na utambulisho wa mwanamke kama unavyojitokeza katika Kifo Kisimani (2001). Sehemu ya kwanza inaangazia nafasi dhalilishi na dunishi. Sehemu ya pili ni nafasi chanya, sehemu ya tatu ni hitimisho. Sura ya nne inaangazia changamoto zinazokabili harakati za kumkomboa mwanamke. Changamoto zenyewe ni za aina aina, kama yanavyodhihirika katika tamthilia hizi. Sura ya tano ina hitimisho ya tasnifu yenyewe. Katika sura yenyewe, kuna ithibati kubainisha kutimia kwa madhumuni ya utafiti wenyewe.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59779
    Citation
    Tasnifu Hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Department of Linguistics and Languages
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback