• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Taswira Ya Mwanamke Katika Tamthilia Zanguzo Mamana Mama Ee

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (323.6Kb)
    Date
    2013-11
    Author
    Chacha, Wilson C
    Type
    Thesis
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tumeangazia taswira ya mwanamke katika tamthilia za Nguzo Mama na Mama Ee. Jamii mbalimbali zina mtazamo anuai kuhusu taswira ya mwanamke. Waandishi wa tamthilia hizi walitoka maeneo tofauti na waliandika katika vipindi tofauti, lakini kazi zao zinashabihiana sana. Tulichagua mada yetu ili kuchambua na kuchanganua tamthilia za Nguzo Mama na Mama Ee kwa sababu ya fani na maudhui yanayoashiria jinsi hali halisi ilivyo katika jamii zetu. Malengo ambayo tumeyaangazia ni jinsi changamoto mbalimbali zinamkabili mwanamke na kumzuia kupata haki, jinsi asasi za kijamii zinavyochangia mwanamke kutopata mafanikio katika harakati zake za kutaka kujikomboa na kuonyesha jinsi baadhi ya waandishi wamemsawiri mwanamke kwa njia mbalimbali kama vile shujaa, mwongo mwoga na kadhalika. Tuliweza kujikita kwenye vitabu hivi viwili tu, Nguzo Mama na Mama Ee isipokuwa pale tulipohitaji kutoa idhibati au mifano zaidi. Dira iliyotuongoza kuangazia mada yetu ni nadharia ya Sosholojia ya Fasihi iliyoasisiwa na Georg Lucaks mwanaitifaki wa Karl Marx. Nadharia hii ya Sosholojia ya Fasihi ni kitengo maalum cha uchunguzi ambacho humulika mahusiano baina sya kazi ya sanaa hasa fasihi, umma na muundo wa kijamii. Baadhi ya changamoto tulizofanikiwa kugundua katika uchambuzi wetu ni matatizo ya unyumba, ubaguzi wa kijana wa jinsia ya kike, mila na desturi katika ndoa, dini katika mahusiano ya kinyumba, mahakama za kiserikali na zile za kijijini, ukosefu wa umoja na ushirikiano, utabaka,na majukumu mengi miongoni mwa zingine. Asasi za kijamii hasa ndoa na tamaduni zilionekana kuchukua nafasi ya vizingiti vikuu na kumfanya mwanamke kuwa na taswira mbalimbali. Kwa mfano mwanamke amechorwa kama mwoga, mwenye chuki na wivu, mwenye tamaa, mwenye mashaka na mdhaifu miongoni mwa nyingine. Tulitamatisha kazi yetu kwa kutoa mapendekezo mawili. Pendekezo la kwanza linahusiana na dini. Swala la dini kuchangia katika unyanyaswaji wa mwanamke yafaa lichunguzwe kwa undani zaidi. Pendekezo la pili linahusiana na suluhu la kudumu kuhusu changamoto zinazomkumba mwanamke katika jamii na kumnyima uhuru kamili.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60086
    Publisher
    University of Nairobi
    Description
    Tasnifu hii imetolewa ili kutosholeza baadhi ya mahitaji Ya uzamili katika chuo kikuu cha Nairobi.
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback