• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Ulinganishi Wa Matumizi Ya Tasfida Za Muktadha Wa Nyumbani Katika Lugha Ya Kikamba Na Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (398.7Kb)
    Date
    2013
    Author
    Nguti, Mary
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii imeshughulika na kulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha ya Kikamba na ya Kiswahili. Ingawa tasnifu hii imetolewa kwa mahitaji ya shahada ya Kiswahili, data iliyochanganuliwa ni kutoka lugha ya Kikamba na ya Kiswahili. Uchanguzi huu tuliufikia kwa kutambua umuhimu unaostahili kupewa lugha zetu nyingine za Kiafrika katika muktadha wa nyumbani na miktadha mingine mbalimbali. Kwa sababu ya juhudi zinazofanywa na kila jamii kuikuza na kustawisha maadili katika maisha ya binadamu wote (Stockwell, 2008). Ndiposa tukawa na jukumu la kuchunguza matumizi ya tasfida za nyumbani. Somo la tasnifu hii ni ulinganishi wa matumizi ya tasfida katika lugha ya Kikamba na Kiswahili katika muktadha wa nyumbani. Tumechunguza matumizi ya tasfida kwa lugha ya Kikamba na kulinganisha na matumizi katika lugha ya Kiswahili. Hatukulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha hizi mbili kwa kutaka kulingamisha tu bali, kwa kufanya hivyo tumetoa mwanga zaidi kuonyesha kuwa, tasfida ni chombo muhimu na maalum cha mawasiliano katika jamii yoyote. Tumeonyesha kwamba jamii mbili zinazotofautiana kwa mengi huweza kuwa na mawazo sawa kuhusu jamii na mazingira yao kwa jumla. Madhumuni makuu katika tasnifu hii yalikuwa kulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha hizi mbili, Kikamba na Kiswahili ili kudhibitisha kuwa, kunao uhusiano mkubwa katika matumizi ya tasfida. Tumechambua jinsi matumizi ya tasfida hufanikisha mawasiliano katika lugha ya Kikamba na Kiswahili. Tulikuwa na shabaha pia ya kuchunguza jinsi hali za jamii kama umri, Kazi, jinsias na hadhi huathini matumizi ya tasfida. vii Data ilikusanywa kupitia mahojiano na hojaji zilijazwa na watafitiwa wateule. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kubainishwa kwa msingi wa nadharia ya Upole iliyoasisiwa na Penelope Brown na Levinson (1978).
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60185
    Citation
    Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Nairobi
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback