• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Mtindo katika diwani ya mfuko mtupu na hadithi nyingine

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (327.4Kb)
    Date
    2013-11
    Author
    Katutu, Ruth M
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii imeshughulikia mtindo katika Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Katika sura ya kwanza, mambo muhimu yanayojadiliwa ni; Utangulizi, Tatizo la Utafiti, Madhumuni ya Utafiti, Nadharia Tete, Sababu za Kuchagua Mada, Upeo na Mipaka ya tasnifu, Msingi wa Nadharia ya Utafiti, Yaliyoandikwa kuhusu mada hii na mwisho ni njia tulizotumia kukamilisha utafiti huu. Katika sura ya pili, utafiti wetu umejikita katika kuchunguza matumizi ya msamiati katika Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Tumeshughulikia jinsi mwandishi ameteua msamiati wake ili kuwasilisha ujumbe anaodhamiria kufikisha kwa hadhira yake. Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa mtindo kwa misingi ya kisintaksia katika Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Tumechunguza ukiushi katika baadhi ya kategoria za maneno. Pia tumejadili ukiushi katika sentensi ndefu, fupi na nafasi ya uakifishaji katika sintaksia ya diwani yenyewe. Tumemalizia sura hii kwa kujadili ukiushi unaoibuka kwa kutozingatia muundo wa kiima kiarifa. Katika sura ya nne, tumechanganua ukiushi wa kisemantiki katika diwani ya kazi hii ya Said Mohamed . Tumechunguza tamathali za usemi kama tashbihi, sitiari, kinaya, tashhisi, tanakuzi, majazi, tasifida, maswali ya balagha na chuku. Pia tumechunguza mbinu nyingine za lugha kama takriri, usambamba wa visawe, tanakali za sauti, kuchanganya ndimi, jazanda, methali, barua na nyimbo. Sura ya tano tumehitimisha kwa kurejelea yale tuliyojadili katika sura za awali hasa kwa kuangaza madhumuni, nadharia tete na nadharia tuliyotumiwa kuhakiki kazi hii. Kadhalika tumeonyesha mchango wetu kutokana na yale ambayo tumeshugulikia katika utafiti huu. Hatimaye, tumetoa mapendekezo yetu kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60231
    Publisher
    University of Nairobi,
     
    Department of Kiswahili
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback