• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchanganuzi Linganishi Wa Sintaksia Ya Sentensi Sharti Ya Kiswahili Sanifu Na Ekegusii

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (534.3Kb)
    Date
    2013
    Author
    Nyandago, Francis O
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Lengo la tasnifu hii ni kufanya uchunguzi linganishi wa sentensi sharti ya Kiswahili Sanifu na Ekegusii kwa kutumia nadharia ya Upanuzi wa Sarufi Sawazishi. Tumeigawa kazi hii katika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumetoa maelezo ya kimsingi yanayohusu somo la utafiti, madhumuni ya utafiti na upeo wa tasnifu. Masuala mengine ambayo yameshughulikiwa ni pamoja na sababu za kulichagua somo, nadharia tete, yaliyoandikwa kuhusu somo hili, msingi wa nadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili inalenga kushughulikia sintaksia ya sentensi sharti ya Kiswahili Sanifu. Sura imeanza kwa kutoa fasili ya sentensi sharti ya Kiswahili na ufafanuzi wa viambajengo vyake. Viambajengo hivi ni pamoja na kishazi sharti, kishazi shurutiwa, vitambulishi sharti na viunganishi viambatishi. Vipashio vinavyotumiwa kutolea masharti vimetambuliwa na kufafanuliwa. Vipashio hivi ni pamoja na ‘kama, ikiwa, endapo, iwapo, ki, nga, ngali, nge na ngeli’. Suala lingine lililoshughulikiwa katika sura hili ni muundo wa sentensi sharti ya Kiswahili na ugeuzi unaojitokeza katika kuigeuza sentensi sharti kutoka kiwango cha muundo msingi hadi kile cha muundo geuzi. Imebainishwa kuwa sentensi sharti ya Kiswahili ikiwa katika kiwango cha muundo msingi huwa na kishazi shurutiwa mwanzoni kikifuatwa na kishazi sharti. Vishazi hivi huunganishwa kwa mujibu wa kitambulishi sharti kinachokitegemeza kishazi sharti kwa kishazi shurutiwa. Sentensi hiyo inapogeuzwa hadi kiwango cha muundo geuzi, kanuni ya ugeuzi hukitanguliza kishazi sharti kikifuatwa na kishazi shurutiwa. Wakati wa ugeuzi huo, kiunganishi kiambatishi kisicho cha lazima hutokea na kukitegemeza kishazi sharti kwa kishazi shurutiwa. Sura ya tatu inashughulikia fasili ya sentensi sharti ya Ekegusii na ufafanuzi wa viambajengo vyake. Viambajengo hivi ni pamoja na kishazi sharti, kishazi shurutiwa, vitambulishi sharti na viunganishi viambatishi. Imebainika kuwa sentensi sharti ya Ekegusii huundwa kwa kishazi sharti na kishazi shurutiwa. Vitambulishi sharti katika lugha ya Ekegusii ni pamoja na ‘onye, -ise, -are, k- na ebe’. Kuna kiunganishi kiambatishi kitumiwacho ambacho si cha lazima kinachotumiwa kukiunganisha kishazi sharti na kishazi shurutiwa. Kiunganishi hiki ni ‘rirorio’ ambacho hudhihirika katika kiwango cha muundo geuzi pekee. Mengine yaliyoshughulikiwa katika sura hii ni muundo wa sentensi sharti ya Ekegusii na ugeuzi unaojitokeza katika kuigeuza sentensi sharti kutoka kiwango cha muundo msingi hadi kile cha muundo geuzi. Uchunguzi umepata kuwa sentensi sharti ya Ekegusii ikiwa katika kiwango cha muundo msingi huwa na kishazi shurutiwa kikitangulia mwanzoni mwa sentensi kikifuatwa na kishazi shurutiwa. Kishazi sharti hutegemezwa kwa kishazi shurutiwa kwa matumizi ya kitambulishi sharti kinachotekeleza pia jukumu la kutambulisha sharti. Sentensi sharti hugeuzwa kutoka kiwango cha muundo msingi hadi muundo geuzi kutokana na ugeuzi unaokitanguliza kishazi sharti kikifuatwa na kishazi shurutiwa. Ugeuzi huo husababisha kutokea kwa kiunganishi kiambatishi ‘rirorio’ kisicho cha lazima na kinachoviunganisha vishazi husika kwa kukitegemeza kishazi sharti kwa kishazi shurutiwa. Katika sura ya nne, ulinganishi wa vipengele mbali mbali vinavyohusiana na sintaksia ya sentensi sharti ya Kiswahili sanifu na Ekegusii umefanywa. Kumeshughulikiwa uainishaji wa sentensi sharti ya Kiswahili na Ekegusii, kufanana na kutofautiana kwa kishazi sharti cha Kiswahili na cha Ekegusii, kufanana na kutofautiana kwa miundo ya sentensi sharti ya Kiswahili na Ekegusii na ulinganishi wa michakato ya ugeuzi inayogeuza sentensi sharti kutoka kiwango cha muundo msingi hadi kile cha muundo geuzi. Sura ya tano inatoa mahitimisho ya kijumla ya tasnifu hii. Inaanganzia masuala muhimu yaliyoshughulikiwa na mahitimisho yao katika kila sura ya tasnifu hii na kisha kutoa mapendekezo kulingana na maoni ya mtafiti.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60461
    Citation
    Master of Arts
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Department of literature and language
     
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback