• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uwazi Na Umaanisho: Usimbaji Maana Kimazungumzo Katika Ekegusii Na Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (278.2Kb)
    Date
    2013
    Author
    Ochichi, Alice K
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti huu ulichunguza jinsi wazungumzaji hutumia misimbo inayozua uwazi na umaanisho katika lugha za Kiswahili na Ekegusii kwa lengo la kubainisha kama kuna mlingano wowote kati ya lugha hizi, zote zikiwa lugha za Kibantu. Lugha hizo zimeelezwa kisemantiki ambapo maana msingi za kauli zimechanganuliwa, na baadaye maana za kipragmatiki kuelezwa kwa kutumia Nadharia ya Uhusiano. Nadharia ya Uhusiano ya Sperber na Wilson (1986) ilitumiwa kufasiri misimbo iliyotokana na kategoria mbalimbali za lugha hizi mbili ambapo kanuni za uhusiano pamoja na kanuni ya ujuzi wa msikilizaji zilisaidia kupata fasiri iliyokusudiwa na wasemaji wa kauli mbalimbali. Tasnifu hii ina sura nne. Katika sura ya kwanza, tumeshughulikia utangulizi kwa jumla. Tumeeleza kuhusu lugha za Kiswahili na Ekegusii, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchangua mada, upeo na mipaka misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada yetu pamoja na mbinu za utafiti tulizotumia. Katika sura ya pili, tumejadili kuhusu kategoria za kisemantiki kwa jumla ambapo tumebainisha makundi mawili makuu ya kisemantiki ambayo ni pamoja na kategoria za kileksika na kategoria za kimuktadha. Sura ya tatu imejadili kategoria mbalimbali za kisemanti ambazo huibuka kimazungumzo katika lugha ya Kiswahili na vilevile lugha ya Ekegusii na kueleza uwazi na umaanisho wa kauli hizo. Ufafanuzi wa maana kiumaanisho umefanywa kwa kutumia mbinu za kinadharia za uhusiano. Nadharia ya Uhusiano ilitumiwa ambapo ilibainika kwamba lugha hizi mbili zinatumia mitindo tofauti kuzua umaanisho. Aidha, tofauti za kiuteuzi wa maneno zimebainishwa katika lugha zote. Sababu za tofauti hizo zimejadiliwa. Katika sura ya nne, mahitimisho na mapendekezo yametolewa ambazo nadharia tete pamoja na madhumuni ya utafiti yametathminiwa. Kutokana na tathmini hizo pamoja na uchanganizi wa data yetu, tumerejelea nadharia tete zetu ambapo baadhi zimekubaliwa na nyingine kukanushwa. Vilevile, katika sura hii tumetoa mapendekezo ya tafiti za baadaye. Uchanganuzi wa misimbo mbalimbali ulidhihirisha tofauti za uteuzi wa kategoria za kisemantiki zinazotumika katika lugha za Kiswahili na Ekegusii, na maana zilizosimbwa pia zilibainisha tofauti kadha wa kadha. Hali hii ilibainishwa na tofauti za fahamu za awali za tamaduni katika lugha hizo mbili, mitazamo pamoja na mazingira ya watumizi wa lugha hizi.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60540
    Citation
    Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi
    Publisher
    University of Nairobi
     
    Idara ya isimu na lugha
     
    Description
    Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya shahada ya uzamili katika kiswahili
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback