• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Matatizo yanayodhihirika katika matini tafsiri za kimatibabu: utafiti kielelezo katika Hospitali ya Kisii level 5

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (8.363Mb)
    Date
    2013
    Author
    Moraa, Lydia
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti wetu unahusu matatizo yanayodhihirika katika matini tafsiri za kimatibabu. Kwa kuwa taaluma ya kimatibabu ni pana, tuliteua sehemu nne za kurejelea katika utafiti huu. Sehemu hizi ni: magonjwa kwa jumla, dalili au ishara za magonjwa, tiba na uzuiaji. Tuliangazia matini zinazohusiana na sehemu tulizotaja kama zinavyodhihirika katika hospitali ya Kisii Level 5. Matatizo tunayorejelea ni ya kiisimu na yale yasiyokuwa ya kiisimu. Katika hospitali ya Kisii Level 5 kuna kikundi kiitwacho ‘Quality Improvement Team’ ambacho hujihusisha na kutafsiri matini hizi. Tafsiri hizi ni za kihuduma na ziko katika mabango, maagizo yaliyoandikwa, maelezo, vijikaratasi vya maelezo na vijitabu. Tafsiri za kimatibabu ni swala linalohitaji uangalifu mkubwa kwa kuwa huathiri afya ya mwanadamu. Kwa sababu ya kuchanganyika kwa watu kutoka jamii mbalimbali, tafsiri husaidia kupitisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine. Wadensjo (1998) anadai kuwa katika nchi nyingine, tafsiri zinazohusiana na sheria, afya na elimu zimeendelezwa kama taaluma za kiusomi (TY). Anaendelea kusema kuwa ni dhahiri kwamba wataalamu wa kimatibabu hawawezi kutoa huduma za kuridhisha za kiafya ikiwa hawawezi kuwasiliana vyema na wateja wao(uk 88, uk88). Hivyo basi tafsiri za kimatibabu ni jambo ambalo haliwezi kufanywa bila umakinifu unaohitajika. Gambier (2001) anadai kuwa tafsiri si kitendo rahisi cha kupitisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine ila ni kitendo changamano kinachohusu uakifishaji, njia za kueleza wakati, tarehe na mahali (TY). Maelezo haya ya Gambier yanawiana vyema na tunachosisitiza kuhusiana na tafsiri za kimatibabu. Vipengele alivyovitaja Gambier kama vile kuzingatia uakifishaji na wakati ni swala muhimu katika tafsiri za kimatibabu. Ushauri wanaotoa wahudumu wa kimatibabu huathiriwa na maelezo na wakati kwa mfano, tiba hasa kuhusu tembe huwa na maelezo ya wakati. Mtafsiri apitishe ujumbe usiokuwa na utata wa maagizo na maelezo katika karatasi za tembe. Badala ya kutaja kuwa tembe zitumike asubuhi, mchana na jioni, ni vyema kutaja wakati mahususi kama saa moja jioni kwa kuwa jioni huanza saa kumi.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/64573
    Citation
    Moraa Lydia (2013). Matatizo Yanayodhihirika Katika Matini Tafsiri Za Kimatibabu: Utafiti Kielelezo Katika Hospitali Ya Kisii Level5
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback