• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Viongozi kama visababishi vya mabadiliko katika riwaya za Mwenda Mbatiah: Vipanyam vya maabara na majira ya tufani

    Thumbnail
    View/Open
    Full-text (550.7Kb)
    Date
    2014
    Author
    Njoroge, Anne W
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Katika utafiti wetu tumeangazia viongozi kama visababishi vya mabadiliko katika riwaya za Vipanya Vya Maabara na Majira Ya Tufani. Jamii mbalimbali huwa na mitazamo anuai kuhusu majukumu ya viongozi na mchango wao hauwezi kupuuzwa. Mwandishi wa riwaya hizi ameangazia majukumu ya viongozi yanayoshabihiana katika kuleta mabadiliko kwenye jamii zake, hivyo basi makala haya yanachunguza mchango wa viongozi kama visababishi vya mabadiliko dhahiri. Tulichagua mada hii ili kuchambua riwaya hizi kwa sababu ya maudhui yanayoashiria jinsi hali halisi ilivyo katika jamii zetu. Malengo ambayo tumeyaangazia ni kuchunguza jinsi matendo ya viongozi yanavyohujumu uchumi wa nchi, kutathmini ikiwa matendo ya viongozi yanaakisi maadili ya kijamii na kupambanua hali za unafiki zinazodhihirika katika matendo ya viongozi. Tulijikita kwenye kazi hizi mbili Vipanya Vya Maabara na Majira ya Tufani pamoja na kurejela kazi zingine ili kutoa idhibati zaidi. Tuliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi iliyoasisiwa na Norman Fairclough, Teun Van Djik na Ruth Wodak miongoni mwa wengine,kwa mitazamo ya Wodak na Reisigl,inayozingatia mkakati wa kurejelea, mkakati wa unominishaji, mkakati wa ubishi, mkakati wa kudhihirisha nguvu za usemi na vilevile mkabala. Baadhi ya mambo yaliyojitokeza katika utafiti wetu ni kwamba mabadiliko yanayoshuhudiwa katika nchi na jamii mbalimbali husababishwa na viongozi. Kwa mfano ufisadi, utabaka, wizi wa kimabavu, hujuma miongoni mwa maovu mengine mengi. Mabadiliko haya yanasababishwa na kuweko kwa uwezo mkubwa wa watawala katika kuwatawala watawaliwa.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/75212
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback