• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Mielekeo ya walimu wa shule za msingi kuhusu suala la lugha kama linavyoelezwa katika katiba ya Kenya

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (912.0Kb)
    Date
    2014
    Author
    Mirianga, Rose Kaumeuru
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Nchini Kenya, walimu wa shule za msingi ni kielelezo cha kuigwa na wanajamii walio wengi hasa katika maeneo ya mashambani. Aghalabu, wanayoyatenda na wanayoyasema walimu hawa kuhusiana na lugha ndiyo yanayofuatwa na wanajamii walio wengi. Tasnifu hii ni uchunguzi wa mielekeo ya wadau hawa muhimu kuhusu majukumu yaliyotengewa lugha mbalimbali, ukuzaji na uendelezaji wa matumizi ya lugha kama inavyoangaziwa na kauli za Katiba ya Kenya zihusuzo suala la lugha. Mielekeo ya wadau hawa inatarajiwa kuwa mwongozo kwa waundaji sera ya lugha na pia wapangaji lugha ili kubuni mikakati ya kuhimiza ushawishi na uhusika wa walimu husika, kama wadau muhimu, katika kutekeleza sera ya lugha kama inavyojitokeza katika Katiba ya Kenya ya mwaka wa 2010. Uchunguzi huu ulijikita nyanjani ambapo data ilikusanywa kwa njia ya hojaji, mahojiano na utazamaji wa tabia za watafitiwa kuhusu lugha ya Kiswahili, Kiingereza na lugha asilia (Kimeru). Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mielekeo ya watafitiwa kuhusu suala la lugha kama linavyojitokeza katika Katiba ya Kenya, imetokana na masiala ya kihistoria, kijamii, kiisimu na kiuchumi. Uchanganuzi wa data ya utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kijamiinafsia iliyoasisiwa na Lambert (1963) na ile ya Kijamii ya Fishman (1972).
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/75310
    Publisher
    University of Nairobi
    Description
    Thesis MA
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback