• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Fonolojia ya nomino-mkopo za kikamba kutoka Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (654.0Kb)
    Date
    2014-11
    Author
    Mulwa, Magdalene N
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti huu umechanganua taratibu za utohozi wa nomino za Kikamba kutoka Kiswahili kwa madhumuni ya kuainisha kanuni zinazohusika. Uchanganuzi umeongozwa na mtazamo wa Fonolojia ya vipande sauti huru ambao ni mojawapo ya mitazamo ya Fonolojia Zalishi. Kulingana na mtazamo huu, fonolojia ni mfumo sauti wenye rusu nne: rusu msingi, rusu fonimu, rusu silabi na rusu toni. Nadharia ya Mawimbi pia ilitumiwa kueleza sababu zilizochangia ukopaji katika lugha ya Kikamba. Utafiti wetu umeainisha nomino za Kikamba zilizokopwa kutoka Kiswahili, ukabainisha vigezo vya kifonolojia vilivyotumika na kuchanganua taratibu na kanuni za kifonolojia zilizofuatwa katika ukopaji huo. Vigezo vya fonolojia ya Kikamba ambavyo ni fonimu, silabi na sifa arudhi vimebainishwa. Pia, sababu zilizochangia ukopaji katika lugha ya Kikamba zimeelezwa. Data msingi ya utafiti ilikusanywa katika sehemu ya Kitui ya kati kupitia mbinu za mahojiano na uchunguzi wa kushiriki. Katika uwasilishaji, maelezo yameambatana na michoro na majedwali. Uchunguzi umedhihirisha kwamba katika kushughulikia maneno mkopo, mbinu tatu huhusika nazo ni: uchopekaji, udondoshaji na ugeuzaji maumbo. Utafiti wetu una nafasi ya kuchangia uwanja wa isimu lugha ya Kiafrika kwa jumla tukizingatia kwamba utohozi unaweza kutumika katika kulinganisha mifano ya fonolojia. Pamoja na haya, data ya matokeo ya uchunguzi wetu inaweza kuwasaidia wasomi wa isimu za lugha za Kiafrika. Vile vile, matokeo ya utafiti huu yanachangia kukua kwa lugha ya Kikamba kwani uchunguzi ulishughulikia mabadiliko yaliyofanyiwa maneno yaliyokopwa na hii ni njia moja ambayo lugha hutumia kukuza msamiati wake
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/75643
    Citation
    Shahada ya uzamili katika idara ya Kiswahili ya chuo kikuu cha Nairobi
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback