• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Nafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto : mtazamo wa fasihi ya ufeministi wa kiekolojia

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (843.7Kb)
    Date
    2014
    Author
    Sabula, Millicent A
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Fasihi ya kiekolojia ni uwanja uliochipuka miaka ya 1970 na kuendelea miaka ya 1990 kuchanganua, kuchambua na kuhakiki kazi za kifasihi. Uwanja huu unalenga kuangazia fani na maudhui katika matawi ya fasihi kiekolojia kama vile ya Kiafrika, Kimarekani na Kifeministi. Utafiti huu unahusu nafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira kwa mtazamo wa fasihi ya ufeministi wa kiekolojia. Lengo kuu la utafiti huu ni kupambanua mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni haya: kubainisha mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto; kupambanua mhusika Nakuruto na mchango anaoutoa katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira; kujadili kwa kina changamoto anazopitia mwanawake katika kuhifadhi mazingira; kujadili athari za masuala ya kimazingira na jinsi zinavyojitokeza katika riwaya. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi wa kiekolojia iliyoasisiwa na mfaransa Francoise d‘Eaubonne mwaka wa 1974. Nadharia hii ilibuniwa kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya kiekolojia hasa kwa kumzingatia mwanamke. Utafiti huu ulifuata muundo wa uchanganuzi wa makala ambapo maelezo yetu yaliangazia masuala tata yaliyoko kwenye matini tuele. Makala ya kimsingi ya utafiti yalikuwa ni riwaya ya Nakuruto ilhali makala ya sekondari yalitokana na usomaji wa vitabu na makala yaliyohusu mada. Utafiti huu ulibainisha kwamba ufeministi wa kiekolojia una nafasi ya kuwazindua wanawake ili kuleta ukombozi wa kimazingira. Aidha, utafiti ulitambua kuwa mhusika Nakuruto aliwazindua wanajamii kupitia kwa elimu na maarifa yake ya kimazingira, hivyo kusababisha mapinduzi. Utafiti ulitambua kwamba wanawake wanasimangwa, kutukanwa, kudharauliwa na kudunishwa wanapojihusisha na harakati za utunzaji mazingira. Mwisho utafiti ulitambua kwamba umaskini, kukauka kwa chemichemi za maji, uskwota, magonjwa na vifo ni athari zinazosababishwa na uharibu wa mazingira. Utafiti huu ulihitimisha kwamba mwanamke anastahili kupewa nafasi katika uhifadhi wa mazingira na kwamba, fasihi ya Kiswahili ina uwezo wa kumulika masuala ya kielokojia kama yanavyojitokeza katika jamii. Kwa kuwa utafiti huu haukuweza kuchunguza vipengele vyote vya kifasihi mazingira, mtafiti anapendekeza kwamba utafiti wa baadaye uzingatie mikabala mingine kama vile fasihi mazingira kieneo, Kiafrika na Kimagharibi, hasa kwa mkondo wa kilinganishi
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/75733
    Citation
    Master of Arts in Kiswahili
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback