• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Matumizi Ya Lugha Katika Kanisa Katoliki: Uchanganuzi Wa Ubadilishaji Msimbo Katika Mahubiri

    Thumbnail
    View/Open
    Full-text (829.3Kb)
    Date
    2014
    Author
    Waweru, Teresia W
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuangalia matumizi ya lugha katika Kanisa Katoliki kwa kuchanganua ubadilishaji msimbo katika mahubiri. Utafiti ulitumia data iliyokusanywa kwa kurekodiwa katika makanisa teule matatu kwa kutumia nadharia ya Umaanisho ya Grice (1975). Tuliongozwa na haipothesia zifuatazo; kwanza, kuwa ubadilishaji msimbo katika diskosi ya mahubiri unaathiri maana katika kiwango cha matumizi ya elementi za kiisimu. Pili, wahubiri katika Kanisa Katoliki hubadilisha msimbo. Tatu ubadilishaji msimbo katika diskosi ya mahubiri husababisha ukosefu wa urasmi na nne kiwango cha elimu, tabaka, tajriba, cheo na umri husababisha mabadiliko ya jinsi lugha inavyotumika. Ilithibitika kuwa ubadilishaji msimbo katika diskosi ya mahubiri unaathiri maana katika kiwango cha matumizi ya elementi za kiisimu, na kwamba wahubiri katika Kanisa Katoliki hubadilisha msimbo kwa wingi katika mahubiri ambapo ubadilishaji huu husababisha ukosefu wa urasmi. Aidha elimu, tabaka, tajriba, cheo na umri husababisha mabadiliko ya jinsi lugha inavyotumika. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia kwa muhtasari kile kinachofanywa katika utafiti huu kwa kutoa mwelekeo jinsi utafiti wenyewe utakavyofanyika. Sura ya pili imeshughulikia ubadilishaji msimbo kwa kuzingatia mbinu na mikakati mbalimbali. Imeshughulikia pia msingi wa ubadilishaji msimbo na aina za ubadilishaji msimbo. Majukumu na athari za ubadilishaji msimbo pia zimezingatiwa. Baadaye ufungamano wa misingi ya ubadilishaji msimbo na Kanisa Katoliki umeshughulikiwa. Sura ya tatu na ya nne zimehusika na uchanganuzi wa data kwa kutumia vijenzi na msingi wa nadharia ya Umaanisho juu ya ubadilishaji msimbo wakati wa mahubiri katika Kanisa Katoliki. Sura ya tano ni hitimisho na muhtasari ambapo tumetoa maoni na mapendekezo.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/75754
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback