• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Hali, Hadhi Na Majukumu Ya Sheng Mjini Nakuru

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (232.3Kb)
    Date
    2014
    Author
    Njoroge, Florence W
    Type
    Thesis; en_US
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Sheng imekuwa moja wapo wa lugha vipindi ambayo inatumika sana kwenye miji mingi nchini Kenya ukiwemo mji wa Nakuru. Matumizi ya lugha hii nyumbani, mitaani na hata shuleni umepelea lugha hii kukua na hata kuongeza misamiati na kuongezeka kwa watumiaji wa lugha hii. Utafiti huu ulilenga kutambulisha hali, hadhi na majukumu ya Sheng mjini Nakuru huku tukilinganisha Sheng na lugha nyingine zinazotumika mjini humo. Sababu ya kuteua mada hii ni kuona kuwa vijana wengi mijini wanatumia Sheng kama kitambulisho chao kilugha na haijatambulika kisheria. Malengo ya kazi hii nikutafiti kama Sheng ina majukumu maalum mjini Nakuru, kama hadhi ya lugha hii ni ya chini na kama kuna tofauti zilizoko katika matumizi ya Sheng kimaeneo. Ukusanyaji wa data kwa ajili ya utafiti huu ulifanywa kwa njia ya hojaji ambayo iliyafumbata maswala ambayo kwa kawaida hupelekea mtuamiaji wa lugha kuonekana kana kwamba ni mtu aliye na uelewa wa lugha tofauti mbali na kuonyesha hadhi zipewazo lugha mjini Nakuru. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia nadharia ya lugha na utambulisho wa jamii ya Gumperz na Cook (1982), nadharia chanzo cha ujifunzaji wa lugha ya pili ya Stephen Krashen (1989) na nadharia ya jumuishi na utambulisho ya Gile (1979). Uchanganuzi kutokana na nadharia hizi umeonyesha kuwa kila lugha huhusishwa na kikundi fulani cha wahusika na lugha hii huwa kama kitambulisho cha jamii husika. Kila lugha hupewa majukumu na hadhi kulingana na watumizi wake ni kina nani. Mbinu za ujifunzaji lugha pia huchangia katika kuipa lugha fulani majukumu na hadhi ya lugha husika. Sheng ni lugha ambayo ni kitambulisho cha vijana wa mijini nchini Kenya ukiwemo mji wa Nakuru
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/75919
    Citation
    (M.A) Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi.
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback