• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Teknolojia ya lugha katika utafiti wa kiswahili: kifani cha mradi wa salama

    Thumbnail
    View/Open
    Fulltext (5.498Mb)
    Date
    2015
    Author
    Gikambi, Hezekiel P
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti wa lugha kuegemea mitazamo ya kikompyuta umetamalaki katika lugha zilizoendelea kidijitali kama Kiingereza na nyinginezo ila dhana hii haijakita mizizi kabisa katika utafiti wa lugha za Kiafrika kama Kiswahili. Utafiti huu umeangazia suala la matumizi ya teknolojia ya lugha katika utafiti wa Kiswahili kwa kuchunguza na kutathmini mbinu mbali mbali zilizotumika katika mradi wa SALAMA (Swahili Language Manager), ulioasisiwa na Arvi Hurskainen profesa wa taaluma za lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Helsinki nchini Finland kutoka 1985- 2015 ili kutambua ukweli wa hali ya utafiti wa Kiswahili katika jukwaa la teknolojia ya lugha. Kwa kutumia mazingira ya SALAMA, ambayo yalishughulikia Kiswahili na kuchunguza nyanja zake mbali kwa kutumia programu zilizojengwa kwenye misingi ya kanuni za lugha na za kikompyuta, utafiti huu ulilenga kubainisha mbinu mbalimbali zilizohusika katika utafiti wa kikompyuta wa lugha ya Kiswahili katika mradi huu na kuzichunguza mbinu hizo zilizotumika kufanyia utafiti na kuchanganulia vipengele tofauti tofauti vya lugha hii, na iwapo zinaweza kuwa zimechangia katika kukuza na kuendeleza utafiti wa Kiswahili kama lugha ya Kiafrika inayoweza kutafitiwa kwa kutumia Teknolojia ya Lugha au Uhandisi Lugha. Katika kufanya hivi, Utafiti umelenga kuonyesha umuhimu, uamilifu na utumiwaji wa kongoo au kopasi katika Teknolojia ya Lugha na jinsi kanzi hii inavyoweza kuboresha utafiti katika lugha ya Kiswahili kikompyuta. Nadharia ya Msambao wa Ugunduzi (Diffusion of Innovation Theory) iliyoasisiwa na Everett Rogers (2003) pamoja na Nadharia ya Isimu Kongoo au Mtazamo wa Kikongoo zimetumika katika kujaribu kueleza jinsi teknolojia ya lugha ni mkabala ulio na manufaa zaidi kiutafiti kuliko mbinu za kimapokeo. Kupitia kwa data kutoka kwa hojaji na mifano kutoka kwa ripoti mbali mbali na kazi za kitaaluma zinazohusu SALAMA, utafiti umebaini kuwa teknolojia ya lugha inachangia katika utafiti ya kiujarabati zaidi, ina uwezo wa kuichakata data kubwa zaidi kikompyuta kuliko uwezo wa binadamu, inampa mtafiti mnepo na uhuru zaidi, inahifadhi lugha kikompyuta na inaweza kushughulikia lugha ya Kiswahili kiutafiti katika maeneo yote kutoka uundaji na utathmini wa kamusi, tafsiri-mashine, uchanganuzi wa kimofolojia, kisintaksia,kisemantiki,ufundishaji lugha na miongoni mwa masuala mengine.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/93216
    Publisher
    University of Nairobi
    Description
    Thesis
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback