• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Ulinganishaji wa fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wataveta na Waswahili

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (2.392Mb)
    Date
    2015
    Author
    Makange, Joseph L
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Nafasi ya fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta ni utafiti wenye gharadhi ya kuonyesha jinsi fani za kiutendi zinavyotumiwa katika nyimbo zinazoimbwa wakati wa harusi.Tulichokusudia kufanya katika utafiti wetu ni kulinganisha fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Malengo ambayo tulikusudia kuangazia ni kubainisha aina mbali mbali za fani za kiutendi,kuonyesha umuhimu wa fani za kiutendi, kubainisha kuwepo au kutokuwepo kwa fani za kiutendi katika nyimbo za harusi na kuonyesha nyimbo mbalimbali zinazoimbwa katika sherehe za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta.Dira iliyotuongoza kuangazia mada yetu ni nadharia ya Sosholojia ya Utendaji iliyoasisiwa na Bronislaw Malinowski kutoka Uholanzi na Radcliffe-Brown kutoka Uingereza.Vile vile tulitumia mtazamo wa viziada lugha wa Okpewho (1992) katika kuelezea fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta.Katika utafiti wetu tuliongozwa na nadharia tete mbili.Kwanza, tulitaka kubainisha ya kwamba fani za kiutendi ni za aina mbalimbali katika jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Pili, tulitaka kudhibitisha ya kwamba fani za kiutendi katika nyimbo za harusi zina uhusiano miongoni mwa jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Mbinu ya utafiti iliyotumiwa ni ile ya sampuli lengwa.Tuliweza kutembelea maktabani na kusoma baadhi ya tasnifu zilizoandikwa.Ushauri wa wahadhiri wetu ulitufaa sana kwani ulikuwa mhimili mkuu wa kazi hii.Utafiti wetu ulimalizikia nyanjani ambapo tuliwahoji watu kumi wenye umri kati ya miaka thelathini hadi themanini(30-80) kutoka katika jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Tulihudhuria harusi tatu kutoka katika jamii hizi na tukachagua nyimbo tano (5) kutoka kila jamii.Utafiti huu umedhihirisha kuwepo kwa uhusiano katika fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii hizi mbili kama vile: minenguo ya mwili,kiitikio,kunyamaza kimya na ishara za uso.Utafiti huu pia umebaini ya kuwa kuna fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii hizi mbili ambazo hazina uhusiano, kama vile: maleba na matumizi ya vidole na mikono
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/93440
    Publisher
    University of Nairobi
    Description
    Thesis
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback