• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchanganuzi Linganishi Wa Maswala Ya Vijana Na Jinsi Yanavyoshughulikiwa Na Waandishi Katika Diwani Ya Tunu Ya Ushairi

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (744.0Kb)
    Date
    2015
    Author
    Nyamemba, Rose
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Katika tasnifu hii tumeonyesha maswala ya vijana na jinsi yanavyoshughulikiwa na waandishi katika diwani ya Tunu ya Ushairi ambayo ina mkusanyiko wa mashairi ya waandishi wanne tofauti.Waandishi hawa ni pamoja na Andanenga, Nyanje, Kiponda na Arege (2013). Utafiti huu umeonyesha kwamba vijana wana changamoto nyingi katika jamii ambazo ni lazima hatua ya dharura ichukuliwe ili kuokoa kizazi kijacho. Tumeshughulikia mashairi kumi na saba ambayo tulichagua kwa kutumia sampuli lengwa. Katika utafiti huu, nadharia ya uhalisia imetumika kuonyesha ukweli wa mambo katika jamii. Ukweli huu ni ule ambao unaweza kuonekana na kuthibitishwa pasi na tashwishi yoyote ile. Nadharia hii ya uhalisia iliwezesha kuhakiki maswala ya vijana katika jamii na jinsi waandishi wa diwani ya Tunu ya ushairi wanavyoshughulikia maswala hayo. Maswala haya ni pamoja na elimu, ukosefu wa maadili, umaskini, magonjwa, ukosefu wa malezi bora na ukosefu wa ajira. Baada ya kufanya utafiti wetu kwa kina tuligundua kwamba ni kweli vijana katika jamii tofauti huwa na changamoto sawa. Pia makisio yetu kuwa waandishi wote katika diwani ya Tunu ya ushairi wana mwelekeo sawa kuhusu vijana ni kweli kwa sababu maswala wanayoyashughulikia ni maswala ibuka katika jamii na yanawahusu vijana.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/93808
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback