• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Mitindo na maudhui katika uchanganuzi wa vibonzo kwenye gazeti la taifa leo

    Thumbnail
    View/Open
    Full text . (13.94Mb)
    Date
    2015
    Author
    Otuoma, Damarice A
    Type
    Thesis
    Language
    Swahili
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Katika utafiti huu tunalenga kuchanganua vibonzo katika gazeti la Taifa Leo. Matumizi ya mikakati ya vibonzo katika diskosi huweza kuzua utata katika kufasiri ujumbe ulionuiwa kumfikia msomaji. Tamko la msemaji au mwandishi fulani huweza kufasiriwa na msomaji kwa njia mbalimbali hasa wanapotumia vibonzo kuwasilisha ujumbe wao. Hali kama hii huibua hisia mbalimbali kulingana na ujumbe ulioko pale na hata kutatua mawasiliano. Utafiti huu ulinuiwa kubaini jinsi ambavyo vibonzo vinavyodhihirika katika kuleta dhana ya Ugatuzi kwenye gazeti la Taifa Leo. Vilevile utafiti huu umenuiwa kuonyesha jinsi mikakati hiyo inavyoathiri ufasiri wa ujumbe unaodhamiriwa na mwandishi wa vibonzo; malengo ya utafiti huu ni kuchanganua vibonzo vinavyobeba maudhui ya Ugatuzi, kuchunguza mbinu ya lugha inayopendelewa sana katika kuwasilishavibonzo hivyo na kuchanganua mitindo ya lugha inayotumika katika utunzi wa vibonzo hivyo. Nadharia ya Utambulisho/ Ujihusishaji ya Giles imetuongoza katika utafiti huu. Data kuhusu vibonzo vinavyoleta dhana ya Ugatuzi vimekusanywa kwa njia ya uchanganuzi wa yaliyomo ambapo nakala 50 za magazeti ya Taifa Leo ya mwaka 2010-2014 zilihusishwa . Mikakati mbalimbali ya kipragmatiki kama vile , matumizi ya jazanda, kinaya, chuku, sitiari, yote yaliweza kubainishwa. Aidha utafiti huu umedhihirisha kuwa matumizi ya kinaya na jazanda katika vibonzo juu ya Ugatuzi ndiyo iko katika kiwango cha juu zaidi kwa asilimia 64% na mengine kuchukua yaliyosalia.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/93905
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback