• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika riwaya ya maisha kitendawili

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (628.3Kb)
    Date
    2015
    Author
    Kilonzo, Peter K
    Type
    Thesis
    Language
    kiswahili
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Dhamira ya utafiti huu ilikuwa ni kuchanganua ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika riwaya ya Maisha Kitendawili ya John Habwe. Mada ilichaguliwa kwa misingi kwamba kazi za kifasihi huibua ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia tofauti. Dira iliyotuongoza kuifanyia utafiti riwaya hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Vuguvugu la ufeministi huwa na nadharia nyingi kama vile Ufeministi wa Uingereza, Ufeministi wa Ufaranza, Ufeministi wa Marekani, Ufeministi wa kibidhaa, Ufeministi wa kitamaduni miongoni mwa aina nyingine. Tuliuteua Ufeministi wa Kiafrika kama msingi wa kuifanyia riwaya hii utafiti kutokana na ukweli kuwa imeandikwa kwa misingi ya Kiafrika. Nadharia hii huonyesha jinsi asasi tofauti katika jamii zinavyopelekea kuwako kwa udhalimu wa kijinsia. Pia, nadharia hii hupendekeza mbinu za kupigania ukombozi wa kijinsia katika jamii. Malengo ambayo tuliyaangalia ni jinsi ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia unaathiriwa na asasi za kijamii, jinsi umri tofauti tofauti unavyoathiri ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika jamii inayomkandamiza mwanamke na ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika kupigania ukombozi. Mbinu tuliyoitumia katika utafiti huu ni ile ya kukusanya matini za data ya utafiti kutoka vitabuni maktabani. Matokeo ya utafiti wetu ni kuwa, asasi za kijamii kama vile utamaduni, siasa, uchumi, dini na jamii hupelekea kuwako wa udhalimu wa kijinsia. Aidha, tuliona kuwa kuna njia mbalimbali zinazotumiwa ili kuleta ukombozi wa kijinsia.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/94555
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback