• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchanganuzi Wa Kimtindo Wa Zinguo La Mzuka Na Mbaya Wetu

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (1.072Mb)
    Date
    2015
    Author
    Nyandiwa, Hudson
    Type
    Thesis
    Language
    Other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Utafiti huu ulihusu uchanganuzi wa kimtindo katika Zinguo la Mzuka na Mbaya Wetu. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza matumizi ya sitiari, chuku, tashbihi, tashihisi, kejeli, tanakuzi na oksimora katika tamthilia zinazohusika. Tulichochewa na ufahamu kwamba mtindo na dhana ya maudhui ni vitengo muhimu vya fasihi ambavyo huandamana na kuegemeana ili kufanikisha dhamira ya mwandishi kwa wasomaji wa kazi yake. Uchochezi huu ulikuwa na ukweli kwamba matumizi ya tamathali za usemi huondoa uchapwa katika kazi za sanaa pamoja na kuwa matumizi ya tamathali za usemi si ya kiajali ila hutumika kimakusudi. Matumizi ya tamathali hizi huwa ni kuwasilisha ujumbe kimuktadha ili kuwezesha uelewa wa matini kwa kina. Utafiti uliongozwa na nadharia ya elimumitindo inayohusu uchanganuzi wa mbinu zote za lugha ambazo hutumika katika mawasiliano ambayo hujumuisha mawasiliano ya fasihi na mawasiliano yasiyokuwa ya fasihi. Ni wazi kuwa tamathali za usemi za sitiari, chuku, tashbihi, tashihisi, kejeli, tanakuzi na oksimora husheheni maana zinapotumika katika muktadha na bila muktadha ni vigumu kuchanganua tamathali yoyote kisemantiki. Kwa hivyo matini huzipa muktadha wa uchanganuzi. Baada ya kuzisoma tamthilia hizi tulitambua kuwa tamathali za usemi tulizotaja hapo juu zilitumika katika tamthilia za Mbaya Wetu na Zinguo la Mzuka. Tulizichanganua kwa kurejelea muktadha wa matumizi yazo kwenye matini hizi. Iligundulika kuwa matumizi ya vipengele vya tamathali za usemi vya sitiari, chuku, tashbihi, tashihisi, kejeli, tanakuzi na oksimora vimechangia katika kuibua, kuendeleza na kuwasilisha maudhui katika tamthilia zinazohusika. Kwa hivyo iligunduliwa kwamba msanii hutawala lugha kiufundi ili kuonyesha tofauti kati ya lugha ya fasihi na lugha ya kawaida. Aidha, tamathali za usemi hutumiwa na msanii kimakusudi. Kwa hivyo ujumbe ulioko kwenye tamathali hizi huwasilishwa kwa kuzingatia muktadha na vilevile, ni vigumu kuchanganua usemi wenye ukiushi ambao hutokea katika hali isiyokuwa na muktadha. Isitoshe, iligundiliwa kwamba ukiushi katika tamathali za usemi huwezesha uelewa wa kina wa matini. Muktadha wa kiisimu huchangia kutoa maana ambayo mwishowe huibua na kuwasilisha maudhui na kwa hivyo kuifanya kazi ya sanaa kuwa na maudhui ya pekee kutokana na ukiushi kwenye usemi huo na mwisho lugha huwa na uwili usioepukika, yaani uwakilishi wa maana ya kisanii na maana ya kimawasiliano. Napendekeza na kutilia mkazo kwamba vipengele vya fani kama vile muundo, wahusika na mandhari vichunguzwe katika tamthilia hizi mbili. Vilevile ukiushi wa kisintaksia, kileksika na wa kisarufi waweza kuchunguzwa. Aidha, nadharia tofauti na tuliyotumia yaweza kutumiwa.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/94804
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback