Show simple item record

dc.contributor.authorGitau, Regina W
dc.date.accessioned2016-04-28T13:35:37Z
dc.date.available2016-04-28T13:35:37Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/95290
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu ni kuchanganua lugha katika sajili ya biashara kwa kutumia mtazamo wa Kipragmatiki. Tumeangazia lugha kimaandishi na kimazungumzo. Kazi hii imegawika katika sehemu tano. Sura ya kwanza imetanguliza kazi yote kwa kuangazia mada ya utafiti. Sura ya tano imetoa muhtasari wa kazi yote. Nadharia tete zifuatazo zimeongoza utafiti huu; maswala yanayoathiri matumizi ya lugha ya matangazo ya biashara ni hadhira inayolengwa na washindani ya kibiashara, lugha inayotumiwa katika matangazo ya biashara hukiuka kaida za mfumo wa lugha kwa lengo la kumnufaisha mtoaji wa matangazo ya biashara, lugha zungumzwa huwa na athari kubwa kutokana na uchochezi wake wa kiakili kuliko lugha andishi kwenye matangazo ya biashara. Uchunguzi wetu tumeufanya kwa kufuata muongozo wa nadharia tatu. Nadharia ya kwanza ni nadharia ya uhusiano iliyoasisiwa na Wilson, D. na Sperber, D. (2004). Nadharia hii imetuongoza kuchunguza ujumbe unaowasilishwa katika matangazo ya biashara na uhusika wa mlengwa katika ujumbe huo. Nadharia ya pili ambayo tumetumia ni ya umaanisho ambayo iliasisiwa na Grice, H.P (1975). Nadharia hii imetuongoza kuchunguza maana katika matangazo ya biashara, huku tukizingatia maana wazi na maana fiche/ ya umaanisho katika matangazo husika. Nadharia ya tatu ni ya vitendo usemi iliyoasisiwa na Justin, J. L (1962). Nadharia hii imetuwezesha kuchunguza utendaji wa lugha katika matangazo ya biashara. Nadharia hizi tatu tumezutumia kwa ushikirikiano yaani zote kwa pamoja. Data yetu kimaandishi tumeipata kutoka kwa jarida la Kilimo Bora, Gazeti la Taifa Leo, matangazo ya biashara kutoka kwa Wizara ya Afya na kwenye mabango. Data kimazungumzo tumeikusanya kutoka soko kuu la vyakula la Thika. Matokeo ya utafiti wetu yamebainisha kuwa lugha katika matangazo ya biashara hutumiwa na mtangazaji kimaksudi ili kumvutia mlengwa. Ushawishi na uchochezi wa kiakili katika lugha ya matangazo ya biashara hufanikisha uwasilishaji na upokezi wa matangazo haya.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleSajili Ya Matangazo Ya Biashara: Mtazamo Wa Kipragmatikien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States