Uchambuzi Linganishi Wa Maudhui Na Mtindo Baina Ya Ngano Za Waswahili Na Wakuria
View/ Open
Date
1987Author
Marwa, Miriam B
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii ni Uchambuzi linganishi wa Mtindo
na maudhui baina ya ngano za Waswahili na Wakuria.
Hivyo basi huu ni uchambuzi wa fasihi simulizi, -ambapo
tunashughulikia ngano peke yake.
Fasihi simulizi inazo tanzu nyingi, baadhi
yake ni nyimbo, vitendawili na ushairi. Tanzu hizi
zaweza kujisimamia zenyewe. Kwa sababu hii hatuwezi
kuzichambua zote kwa pamoja. Hata hivyo ni muhimu kujua
kwamba, tanzu za fasihi sLruu l.Lz L huingiliana. Kwa
mfano katika ngano kuna nyimbo mara kwa mara.
Mahusiko yetu katika ngano hizi, ni kuchambua
maudhui na mtindo. Tusemapo mtindo, tunamaanisha
usanifu wa lugha inayotumiwa na wasimulizi wa ngano ili
waweze kuwasilisha ujumbe wao kwa wasikilizaji. Maudhui
kwa upande mwingine ni ule-ujumbe unaotolewa kwa ajili
ya jamii. Kwa kuwa fasihi simulizi kama fasihi andishi
inamhusu binadamu, kigezo tutakachotumia kupimia kazi
hii ni msingi wa nadharia ya ki-Marx.
Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unaeleza
mahusiko yetu katika tasnifu hii. Pia inaonyesha sababu
za kulichagua somo hili, yaliyoandikwa kuhusu mada ya
kazi hii na njia za utafiti zilizotumiwa kufanya utafiti
wenyewe.
Sura ya pili ni uchambuzi wa ngano za Waswahili
na Wakuria. Kabla ya uchambuzi, kuna utagulizi ambao
unaeleza mahusiko yetu katika sura hii, pamoja na
kueleza kwa muhtasari tu, uhusiano ulioko baina ya mtindo
na maudhui.
Baada ya utangulizi huo, tunaingilia uchambuzi
wenyewe. Uchambuzi huu, umegawanyika katika sehemu
mbili. Sehemu ya kwanza imechukuauchambuzi. wa ngano za
Waswahili. Ngano hizi ni kama zifuatavyo;
(1) Sungura na Fisi
(2) Kinungu Maria
(3) Mtu na Mkewe
Sehemu ya pili imechuk~a uchambuzi wa ngano za
Wakuria. Ngano hizi ni kama zifuatavyo;
(1) Mama na Sungura
(2) Wesanganache
(3) Nyanya na watoto
Sura ya tatu ni ulinganismwa maudhui na mtindo
wa ngano ambazo tumezichambua. Kabla ya ulinganishi
wenyewe. Kuna utangulizi ambao unaeleza sababu za kuwa
na ulinganishihuu. Ulinganismhuu umegawanyika katika
sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza imechukua kufanana kwa maudhui
na mtindo baina ya ngano za Waswahili na Wakuria. Sehemt
ya pili imechukuwa tofauti zilizokobaina ya ngano za
jamii hizi, tukizingatia maudhui na mtindo.
(vii)
Baada ya ulinganishi huu, tuna hitimisho.
Katika hitimisho uamzi na mapendekezo yetu yanajitokeza
Mwisho kabisa kuna ambatisho ambalo ni uambatanishi
wangano zote tulizozichambua. Ngano hizi zimepangwa
kama ifuatavyo; kwanza kuna ngano za Waswahili,
zikifuatiwa na ngano za Wakuria katika lugha ya Kikuria.
Mwisho ni tafsiri ya ngano za Wakuria katika lugha
ya Kiswahili.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [770]
The following license files are associated with this item: