Show simple item record

dc.contributor.authorMarwa, Miriam B
dc.date.accessioned2021-09-27T06:04:39Z
dc.date.available2021-09-27T06:04:39Z
dc.date.issued1987
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155520
dc.description.abstractTasnifu hii ni Uchambuzi linganishi wa Mtindo na maudhui baina ya ngano za Waswahili na Wakuria. Hivyo basi huu ni uchambuzi wa fasihi simulizi, -ambapo tunashughulikia ngano peke yake. Fasihi simulizi inazo tanzu nyingi, baadhi yake ni nyimbo, vitendawili na ushairi. Tanzu hizi zaweza kujisimamia zenyewe. Kwa sababu hii hatuwezi kuzichambua zote kwa pamoja. Hata hivyo ni muhimu kujua kwamba, tanzu za fasihi sLruu l.Lz L huingiliana. Kwa mfano katika ngano kuna nyimbo mara kwa mara. Mahusiko yetu katika ngano hizi, ni kuchambua maudhui na mtindo. Tusemapo mtindo, tunamaanisha usanifu wa lugha inayotumiwa na wasimulizi wa ngano ili waweze kuwasilisha ujumbe wao kwa wasikilizaji. Maudhui kwa upande mwingine ni ule-ujumbe unaotolewa kwa ajili ya jamii. Kwa kuwa fasihi simulizi kama fasihi andishi inamhusu binadamu, kigezo tutakachotumia kupimia kazi hii ni msingi wa nadharia ya ki-Marx. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unaeleza mahusiko yetu katika tasnifu hii. Pia inaonyesha sababu za kulichagua somo hili, yaliyoandikwa kuhusu mada ya kazi hii na njia za utafiti zilizotumiwa kufanya utafiti wenyewe. Sura ya pili ni uchambuzi wa ngano za Waswahili na Wakuria. Kabla ya uchambuzi, kuna utagulizi ambao unaeleza mahusiko yetu katika sura hii, pamoja na kueleza kwa muhtasari tu, uhusiano ulioko baina ya mtindo na maudhui. Baada ya utangulizi huo, tunaingilia uchambuzi wenyewe. Uchambuzi huu, umegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza imechukuauchambuzi. wa ngano za Waswahili. Ngano hizi ni kama zifuatavyo; (1) Sungura na Fisi (2) Kinungu Maria (3) Mtu na Mkewe Sehemu ya pili imechuk~a uchambuzi wa ngano za Wakuria. Ngano hizi ni kama zifuatavyo; (1) Mama na Sungura (2) Wesanganache (3) Nyanya na watoto Sura ya tatu ni ulinganismwa maudhui na mtindo wa ngano ambazo tumezichambua. Kabla ya ulinganishi wenyewe. Kuna utangulizi ambao unaeleza sababu za kuwa na ulinganishihuu. Ulinganismhuu umegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza imechukua kufanana kwa maudhui na mtindo baina ya ngano za Waswahili na Wakuria. Sehemt ya pili imechukuwa tofauti zilizokobaina ya ngano za jamii hizi, tukizingatia maudhui na mtindo. (vii) Baada ya ulinganishi huu, tuna hitimisho. Katika hitimisho uamzi na mapendekezo yetu yanajitokeza Mwisho kabisa kuna ambatisho ambalo ni uambatanishi wangano zote tulizozichambua. Ngano hizi zimepangwa kama ifuatavyo; kwanza kuna ngano za Waswahili, zikifuatiwa na ngano za Wakuria katika lugha ya Kikuria. Mwisho ni tafsiri ya ngano za Wakuria katika lugha ya Kiswahili.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUchambuzi Linganishi Wa Maudhui Na Mtindo Baina Ya Ngano Za Waswahili Na Wakuriaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States