Mielekeo Ya Watawala Wakuu Na Wahadhiri Wa Chuo Kikuu Cha Nairobi Kuhusu Kiswahili Kama Lugha Rasmi Na Ya Taifa Na Athari Zake.
Abstract
Tasnifu hii ni utafiti wa mielekeo ya wakuu na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi kuhusu Kiswahili kama lugha rasmi na ya taifa.Mielekeo yao inatarajiwa kuwaongoza wapangaji wa sera ya lugha ili kubuni njia na mbinu za utekelezwaji wa majukumu rasmi na kukipa Kiswahili nafasi yake katika utekelezaji wa majukumu rasmi na ya kitaifa.Utafiti wa kina ulifanywa nyanjani tulipopata data msingi tuliyoikusanya kwa kutumia hojaji,utazanaji wa wahojiwa na mahojiano kubaini namna wanavyotumia Kiswahili, kikiwemo Kiingereza pamoja na lugha zingine chuoni ili kujua masiala yanayosababisha mielekeo iliyopelekea kuondolewa kwa Idara ya Kiswahili chuoni. Kulingana na matokeo ya utafiti huu, watafitiwa walibainisha kuwa wanafahamu Kiswahili kama lugha rasmi na ya taifa lakini urasimi wa Kiswahili katika utekelezaji wa majukumu rasmi haujatambuliwa. Mielekeo ya watafitiwa kuhusu Kiswahili kama lugha rasmi na ya taifa imetokana na masiala ya kiisimu, kihistoria, kiuchumi na kijamii. Katika uchanganuzi wa data tuliongozwa na nadharia ya makutano na mwachano ya Giles (1982)
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Education (FEd) [6059]
The following license files are associated with this item: