Uforensiki Katika Najisikia Kuua Tena
View/ Open
Date
2024Author
Musiori, Nyagetiria J
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu unashughulikia uforensiki katika Najisikia Kuua Tena (1984). Riwaya hii iliteuliwa kimakusudi ili kupata data toshelevu iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya kimsingi ya utafiti ilitokana na uchanganuzi wa vifaa, mbinu na mikakati mbalimbali ya wahusika katika upelelezi wa matukio ya kihalifu katika riwaya teule. Matukio ya uhalifu yalichunguzwa kwa kina huku vifaa vilivyotumika kutekeleza shughuli ya uhalifu na vilivyotumika kwa upelelezi ili kuwabaini washukiwa vikiangaziwa. Utafiti huu ulitekelezwa katika misingi ya Nadharia ya Chembechembe za Ushahidi iliyoasisiwa na Edmond Locard (1920) na baadaye kuendelezwa na David Holdings (2020). Nadharia hii ilituongoza kutambua jinsi chembechembe za ushahidi zinazopatikana katika eneo la uhalifu zinavyoweza kuwa amana kubwa katika kupeleleza na kuwakamata wahalifu, na vile vile mwelekeo wa kiuchunguzi unaopaswa kuzingatiwa.
Lengo la kwanza la utafiti huu lilihusu kuchunguza uhalifu unavyodhihirika katika riwaya teule. Ilibainika kuwa yapo matukio mengi ya kiuhalifu yaliyofungamana na sehemu, nyakati, sababu na wahusika wa matukio hayo. Lengo la pili lilikuwa kubaini vifaa vilivyotumika katika uhalifu. Vifaa hivi kama alivyoeleza Locard (1920) na Holdings (2020) vilikuwa ithibati tosha ya matukio ya kiuhalifu. Lengo la tatu basi likawa kuvichunguza vifaa na mbinu za kiupelelezi kutegemea mtagusano wa wahalifu na mahali na vifaa vilivyotumika katika kufanikisha kukamatwa kwao. Ilibainika kuwa kwa kiwango kikubwa, maendeleo ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano yalifanikisha kuwakamata wahalifu.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [1015]
The following license files are associated with this item:

