Show simple item record

dc.contributor.authorMusiori, Nyagetiria J
dc.date.accessioned2026-03-17T08:29:08Z
dc.date.available2026-03-17T08:29:08Z
dc.date.issued2024
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/168211
dc.description.abstractUtafiti huu unashughulikia uforensiki katika Najisikia Kuua Tena (1984). Riwaya hii iliteuliwa kimakusudi ili kupata data toshelevu iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya kimsingi ya utafiti ilitokana na uchanganuzi wa vifaa, mbinu na mikakati mbalimbali ya wahusika katika upelelezi wa matukio ya kihalifu katika riwaya teule. Matukio ya uhalifu yalichunguzwa kwa kina huku vifaa vilivyotumika kutekeleza shughuli ya uhalifu na vilivyotumika kwa upelelezi ili kuwabaini washukiwa vikiangaziwa. Utafiti huu ulitekelezwa katika misingi ya Nadharia ya Chembechembe za Ushahidi iliyoasisiwa na Edmond Locard (1920) na baadaye kuendelezwa na David Holdings (2020). Nadharia hii ilituongoza kutambua jinsi chembechembe za ushahidi zinazopatikana katika eneo la uhalifu zinavyoweza kuwa amana kubwa katika kupeleleza na kuwakamata wahalifu, na vile vile mwelekeo wa kiuchunguzi unaopaswa kuzingatiwa. Lengo la kwanza la utafiti huu lilihusu kuchunguza uhalifu unavyodhihirika katika riwaya teule. Ilibainika kuwa yapo matukio mengi ya kiuhalifu yaliyofungamana na sehemu, nyakati, sababu na wahusika wa matukio hayo. Lengo la pili lilikuwa kubaini vifaa vilivyotumika katika uhalifu. Vifaa hivi kama alivyoeleza Locard (1920) na Holdings (2020) vilikuwa ithibati tosha ya matukio ya kiuhalifu. Lengo la tatu basi likawa kuvichunguza vifaa na mbinu za kiupelelezi kutegemea mtagusano wa wahalifu na mahali na vifaa vilivyotumika katika kufanikisha kukamatwa kwao. Ilibainika kuwa kwa kiwango kikubwa, maendeleo ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano yalifanikisha kuwakamata wahalifu.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUforensiki Katika Najisikia Kuua Tenaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States