• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Udhalimu dhidi ya wahusika wa kike katika tamthilia za kiswahili

    Thumbnail
    Date
    2006
    Author
    Kalota, Elizabeth
    Type
    Thesis
    Language
    other
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kulishughulikia suala la udhalimu dhidi ya wahusika wa kike kama linavyojitokeza katika kazi za waandishi wa jinsia zote katika tamthilia za Kiswahili. Waandishi wa kike ni Penina Muhando, Hatia (1972) na Ari Katini Mwachofi, Mama ee (1987). Waandishi wa kiume nao ni A.S. Yahya na David Mulwa, Buriani (1983) na Said Ahmed Mohamed, Kitumbua Kimeingia Mchanga (2000). IIi kulifikia lengo letu, tulishughulikia tamthilia nne zilizoandikwa na waandishi wa kike na wa kiume na kuzichanganua. Pia tulipitia kazi mbalimbali zinazohusiana na mada ya utafiti iii kujifahamisha na masuala yanayohusu wanawake. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha ufeministi ambao ni ufeministi wa Kiafrika. Hii ni nadharia inayojaribu kueleza matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiafrika, kinachoyasababisha najinsi wanavyoweza kujiepusha nayo. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba, mwanamke anadhulumiwa na mifumo ya kiume katika taasisi ambazo zinajikita katika misingi ya ubabe - ume. Pia, yalibainisha kuwa udhalimu unaomkabili mwanamke una leta athari hasi kwa mwanamke na hata kwa jamii nzima. Mapendekezo ya utafiti huu yanaitaka jamii nzima kushirikiana iIi kumaliza udhalimu dhidi ya wanawake. Wanawake wanahimizwa kuwa katika mstari wa mbe\e iIi waweze kuutambua udhalimu dhidi yao na kupambana iIi kujikomboa. Utafiti wa baadaye kuhusu suala la udhalimu dhidi ya wahusika wa kike umependekezwa. Utafiti huo utachangia katika kulimulika suala hili kwa njia nyingine kwa lengo la kutafuta ukombozi kwa wahusika wa kike. Tasnifu hii imegawika katika faslu tano. Kila faslu imejadili kipengee maalum juu ya udhalimu dhidi ya wahusika wa kike. Kunatolewa hitimisho katika kila faslu ambapo msimamo na maoni ya tasnifu yanatolewa kwa mujibu wa yaliyojitokeza katika utafiti. Faslu ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti pamoja na nadharia tete zimeshughulikiwa. Aidha, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo hili pamoja na njia za utafiti zimeshughulikiwa. Faslu ya pili inashughulikia aina mbalimbali za udhalimu dhidi ya wahusika wa kike kama zinavyojitokeza katika kazi zilizoshughulikiwa pamoja na sababu zinazoleta udhalimu huo. Faslu ya tatu inabainisha athari za udhalimu dhidi ya wanawake. Athari ambazo zimejadiliwa ni pamoja na kusambaratika kwa ndoa, kuasi dini, woga, vifo na kukata tamaa. Katika faslu ya nne, mitazamo tofauti ya waandishi wa kazi zilizoshughulikiwa imeangaziwa iIi kuonyesha ulinganifu na tofauti zinazojitokeza kati ya waandishi wa jinsia zote. Faslu ya tano ni mahitimisho ambapo muhtasari wa matokeo ya utafiti, mapendekezo pamoja na tafiti za baadaye zimeshughulikiwa.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18441
    Citation
    Master of Arts
    Publisher
    University of Nairobi.
     
    Department of Kiswahili
     
    Collections
    • Faculty of Education (FEd) [6069]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback