Mtindo unavyoendeleza maudhui katika natala
Abstract
Utafiti huu unahusu jinsi mtindo unavyoendeleza maudhui katika Natala (1997) ya Kithaka Wa
Mberia. Tumeshughulikia vipengele vya kimtindo vya wahusika, matumizi ya lugha na maudhui
katika ujenzi na uendelezaji wa ukombozi wa wanawake katika jamii iliyotawaliwa na mfumo wa
ki-ubabedume unaojitokeza katika Natala. Tumetumia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika
kuchanganulia masuala ya mwanamke, na nadharia ya umuundo kuchunguza vipengele vya
kimtindo.
Kazi yetu imegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza tumejadili somo la utafiti,
madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, nadharia tete, misingi ya
nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti.
Katika sura ya pili tumeshughulikia historia fupi ya tamthilia, awamu za maendeleo ya tamthiliakipindi
cha kabla ya ukoloni, kipindi cha ukoloni na baada ya ukoloni. Aidha tumeshughulikia
muhtasari wa Natala.
Katika sura ya tatu tumechunguza mchango wa wahusika katika ujenzi na uendelezaji wa
maudhui. Tumeangazia dhana ya wahusika, wahusika wakuu na wahusika wadogo, ulinganuzi wa
wahusika, umakundi wa wahusika na dhima yao katika ujenzi wa maudhui.
Sura ya nne imeshughulikia matumizi ya tamathali za usemi na kunga za fasihi na athari zake
katika kuendeleza maudhui. Aidha tumechunguza mandhari yalivyohusishwa na matukio katika
ujenzi na uendelezaji wa maudhui.
Sura ya tano ni hitimisho la utafiti wetu. Tumejadili muhtasari wa matokeo na mapendekezo ya
utafiti wa baaadaye.
Citation
Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi, 013Publisher
University of Nairobi linguistic and languages