Show simple item record

dc.contributor.authorKanyua, Murungi G
dc.date.accessioned2013-11-25T09:33:21Z
dc.date.available2013-11-25T09:33:21Z
dc.date.issued2013-11
dc.identifier.citationShahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi, 013en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59975
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu jinsi mtindo unavyoendeleza maudhui katika Natala (1997) ya Kithaka Wa Mberia. Tumeshughulikia vipengele vya kimtindo vya wahusika, matumizi ya lugha na maudhui katika ujenzi na uendelezaji wa ukombozi wa wanawake katika jamii iliyotawaliwa na mfumo wa ki-ubabedume unaojitokeza katika Natala. Tumetumia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika kuchanganulia masuala ya mwanamke, na nadharia ya umuundo kuchunguza vipengele vya kimtindo. Kazi yetu imegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza tumejadili somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, nadharia tete, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili tumeshughulikia historia fupi ya tamthilia, awamu za maendeleo ya tamthiliakipindi cha kabla ya ukoloni, kipindi cha ukoloni na baada ya ukoloni. Aidha tumeshughulikia muhtasari wa Natala. Katika sura ya tatu tumechunguza mchango wa wahusika katika ujenzi na uendelezaji wa maudhui. Tumeangazia dhana ya wahusika, wahusika wakuu na wahusika wadogo, ulinganuzi wa wahusika, umakundi wa wahusika na dhima yao katika ujenzi wa maudhui. Sura ya nne imeshughulikia matumizi ya tamathali za usemi na kunga za fasihi na athari zake katika kuendeleza maudhui. Aidha tumechunguza mandhari yalivyohusishwa na matukio katika ujenzi na uendelezaji wa maudhui. Sura ya tano ni hitimisho la utafiti wetu. Tumejadili muhtasari wa matokeo na mapendekezo ya utafiti wa baaadaye.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleMtindo unavyoendeleza maudhui katika natalaen
dc.typeThesisen
local.publisherlinguistic and languagesen


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record