• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Education (FEd)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uhakiki wa haini kama riwaya ya kihistoria

    Thumbnail
    Date
    2007
    Author
    Simon, Esther N
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii ni uhakiki wa riwaya ya Haini (2002) kama riwaya ya kihistoria. Tumetumia nadharia ya uhistoria mpya kuyachambua masuala kadha wa kadha katika riwaya. Tasnifu hii ina jumla ya sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi au pendekezo la utafiti wetu. Hapa tumeeleza malengo yetu katika utafiti huu, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada hii, mipaka na upeo, nadharia tete, yaliyoandikwa kuhusu mada hii, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Katika sura ya pili tumehakiki dhana ya usukukaji. Hapa tumetoa utangulizi, msingi wa kazi hadithi ya Haini kwa kifupi, usukaji katika Haini ambao unaenda sambasamba na masuala mengi kama vile mivutano ya kisiasa, ubinafsi, matabaka, mandhari na wakati,uhusiano wa kiutawala na udhalimu, hali ya maisha yajamii, historia fupi ya Zanzibar na mapinduzi. Sura ya tatu ni uhusika na wahusika wa kihistoria katika riwaya ya Haini. Hapa tumeeleza sifa bainifu zinazoakisi uhalisia wa kihistoria ya Zanzibar. Sura yanne ni hitimisho ya tasnifu yote. Hapa masuala muhimu yanayojitokeza katika sura zilizotangulia yanazungumziwa kwa jumla. Hapa kuna utanguiizi, upimaji wanadharia tete na maoni kwajumla. Hatimaye tumetoa uamuzi unaotokana na uhakiki wetu kuhusu kazi hii ya Shafi. Aidha tumeeleza umuhimu na mchango wa tasnifu yetu na kutoa mapendekezo kuhusu yale ambayo tunaonelea yanaweza kufayiwa utafiti zaidi. Tanbihi zinapatikana mwisho wa kila sura. Marejeleo ya tasnifu yote yanapatikana mwisho kabisa baada ya hitimisho.
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/6344
    Publisher
    University of Nairobi, CEES, Kenya
    Subject
    Swahili literature
    Description
    (data migrated from the old repository)
    Collections
    • Faculty of Education (FEd) [6069]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback