• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    `Matatizo Ya Ukalimani:uchambuzi Wa Mahubiri Ya Kidini`

    Thumbnail
    View/Open
    Full-text (1.750Mb)
    Date
    1998
    Author
    Ogonda, Joshphine O
    Type
    Thesis
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Tasnifu hii inashughulikia matatizo ya ukalimani ambapo kwa kuchambua mahubiri ya kidini, tumeweza kuyabainisha baadhi ya inatatizo hayo. Kazi yenyewe imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi. Katika utangulizi wa sura hii tumeweza kutoa maelezo mafupi kuhusu historia ya ukalimani. Tumezungumzia pia kuhusu somo la utafiti, madhumuni ya tasnifu na haipothesia zilizotuongoza katika utafiti wetu. Zaidi ya hayo tumeweza kuangalia yaliyoandikwa kuhusu somo hili ambapo tuliweza kupitia kazi zilizoandikwa kuhusu tafsiri na ukalimani. Vilevile tumeweza kutoa sababu zetu za kuchagua somo hili, msingi wa kinadharia na upeo wa tasnifu. Hatimaye tumeweza kueleza njia tulizotumia katika utafiti wetu. Sura ya pili inazungumzia masiala mbalimbali kuhusiana na ukalimani. Katika sura hii tumeweza kuangalia dhana ya ukalimani na kuilinganisha na tafsiri. Kwa kufanya hivyo tumeweza kuona tofauti na ushabihiano ulioko kati ya dhana hizi mbili. Mwisho tumeangalia aina mbalimbali za ukalimani. Sura ya tatu inahusu uchambuzi halisi wa data tuliyokusanya. Katika sura hii tumezingatia matatizo ya kiisimu katika viwango vinne: fonolojia, sintaksia, leksia na maana. Tuinetoa mifano kuonyesha vile makosa yanavysjitokeza katika kila kiwango. Sura ya nne inashughulikia matatizo yasiyo ya kiisimu. (iv) Hapa turaejaribu kuoanisha matatizo haya na yale ya kiisumu ili kuona vile matatizo yasiyo ya kiisimu yanavyoweza kuchangia yale ya kiisimu. Sura ya tano ni hitimisho. Katika sura hii tumetoa maelezo ya kijumla kuhusu utafiti wetu na matokeo yake. Pamoja na hayo, tumetoa mapendekezo.
    URI
    http://hdl.handle.net/11295/64936
    Citation
    Master of Arts in Kiswahili,
    Publisher
    University of Nairobi,
    Collections
    • Faculty of Arts & Social Sciences, Law, Business Mgt (FoA&SS / FoL / FBM) [24587]

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Useful Links
    UON HomeLibrary HomeKLISC

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2022 
    University of Nairobi Library
    Contact Us | Send Feedback